bongo satellite.: Duniani-michezo.
Breaking News
Loading...
Showing posts with label Duniani-michezo.. Show all posts
Showing posts with label Duniani-michezo.. Show all posts

Thursday, 29 September 2016

TBT: Picha za utoto za mchezaji ghali zaidi duniani Paul Pogba.


Leo Septemba 29 2016 naomba nikusogezee TBT Picha za utoto za mchezaji ghali zaidi duniani Paul Pogba.
Kama humfahamu Paul Pogba ni jamaa ambaye alizaliwa  Lagny-sur-Marne wazazi wake wakiwa wametokea Guinea, katika soka Pogba ana ndugu zake wawili ambao wote wanacheza soka pia, kaka yake Mathias anachezea timu ya taifa yaGuinea.
pogba-chelsea-gossip-584530
pogba-chelsea-gossip-584530Paul Pogba muonekano wake wa sasa
paul-pogba-cropped_1jky8cmzo15yg1jslg427x46bq
paul-pogba-cropped_1jky8cmzo15yg1jslg427x46bqPaul Pogba muonekano wake wa sasa
3682dd0d00000578-3703792-image-a-58_1469213004031
3682dd1600000578-3703792-image-a-61_1469213022135
Pogba wa pili kutoka kushoto waliosimama
105441287-pogba-family-grotto-sport-xlarge_transytkw4dzbcpm_hy4t4hqwrephi_e1tpoik75cayqidp0
Pogba wa katikati na kaka zake
pogba-2-890x395_c
Pogba wa kwanza kushoto
105441290-pogba-family-sport-large_transpvlberwd9egfpztclimqf2tt0gk_6efzt336f62ei5u
Pogba wa kwanza kushoto

Europa League: Manchester United kukabiliana na Zorya Luhansk.


Manchester UnitedImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionManchester United wako nafasi ya mwisho katika ligi ya yuropa baada ya kupoteza katika mechi ya ufunguzi dhidi ya Feyenoord
Kukutana na klabu ya Manchester United katika uwanja wa Old Trafford katika ligi ndogo ya klabu bingwa Ulaya, Europa League, siku ya Alhamisi itakuwa ya 'kuogofya' amesema meneja Yuriy Vernydub wa klabu ya Zorya Luhansk ya Ukraine.
Mechi hiyo itaanza saa nne na dakika tano usiku Afrika Mashariki.
Klabu hiyo ya Zorya Luhansk, ilimaliza katika nafasi ya nne katika ligi ya Ukraine msimu uliopita na wanaanza mechi yao ya kwanza katika hatua ya makundi.
''Hakuna sababu ya kujiepusha. Tunaelewa kwamba Manchester United ni klabu ya kimataifa,'' amesema Vernydub.
Nahodha wa United Wayne Rooney alikuwa anatarajiwa kujiunga katika kikosi cha kwanza cha watu kumi na moja lakini amekuwa na shida ya mgongo.
Wayne RooneyImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionWayne Rooney
Mshambuliaji huyo,30, aliachwa nje katika mechi iliyochezwa wikendi iliyopita katika ligi ya premia waliyoondoka na ushindi dhidi ya Leicester City.
Meneja Jose Mourinho amesema: ''Nilikuwa nimeamini kumchezesha kutoka mwanzo (siku ya Alhamisi) lakini kwa jinsi mambo yalivyo hivi karibuni sina uhakika.''
Mourinho amethibitisha mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic, ataanza katika wachezaji 11 wa kwanza, lakini mashetani hao wekundu watamkosa kiungo wa kati Henrikh Mkhitaryan, huku Luke Shaw akiwa hajulikani hali yake baada ya kurudishwa nyumbani siku ya Jumatano kutokana na maradhi.

Mechi nyingine zitakazochezwa leo

  • Fenerbahçe v Feyenoord - Ulker Stadyumu
  • Machester Utd v Zorya Luhansk - Old Trafford
  • Fiorentina v FK Qarabag- Artemio Franchi
  • Slovan Liberec v PAOK Salonika- U Nisy
  • Hapoel Be'er Sheva dhidi ya Southampton-Yaakov Turner Toto Stadium
  • Sparta Prague v Inter Milan-Generali Arena
  • FC Zürich v Osmanlispor -Letzigrund Stadion
  • Steaua Buc v Villarreal-National Arena
  • FC Astana v BSC Young Boys-Astana Arena
  • Olympiakos v Apoel Nic- Georgios Karaiskakis Stadium
  • FK Qabala v 1. FSV Mainz 05- Bakcell Arena
  • Saint-Étienne v Anderlecht-Stade Geoffroy-Guichard
  • Dundalk v M'bi Tel-Aviv- Tallaght Stadium
  • Zenit St P v AZ Alkmaar-Petrovski Stadium
  • FK Austria Vienna v Viktoria Plzen-Ernst-Happel-Stadion
  • Roma v Astra Giurgiu-Olimpico
  • Ath Bilbao v Rapid Vienna-San Mamés
  • KRC Genk v Sassuolo- Cristal Arena
  • Ajax v Standard Liege- Amsterdam ArenA
  • Celta Vigo v Panathinaikos- Balaídos
  • KAA Gent v Konyaspor- Ghelamco Arena
  • Shakt Donsk v Sporting Braga- Arena Lviv
  • Schalke v FC RB Salzb- VELTINS-Arena
  • FK Krasnodar v Nice -Kuban Stadium
  • bbc.

Kakake Benteke kutocheza miezi mitatu Crystal Palace.

Jonathan Benteke

Image copyrightPA
Image captionJonathan Benteke alijiunga na Crystal Palace kwa mkataba wa mwaka moja
Mshambuliaji wa Crystal Palace Jonathan Benteke, atasalia nje ya uwanja kwa miezi mitatu hadi minne kutokana na jeraha la goti.
Mbelgiji huyo mwenye umri wa miaka 21 , kakake mdogo Christian Benteke, ameshiriki mechi moja klabu hiyo tangu alipojiunga nao rasmi mwezi Agosti.
Meneja Alan Pardew amesema habari kuhusiana na jeraha hilo zilikuwa za ''kukasirisha,'' kwa klabu hiyo na hata wachezaji.
Pardew, ambaye timu yake itacheza dhidi ya Everton katika mechi ya ligi ya Premia siku ya Ijumaa, alisema: '' Shida ya jeraha la goti ndiyo shida kuu.''

Saturday, 24 September 2016

Pambano la Tyson dhidi ya Klitschko laahirishwa.

Pambano lilitarajiwa Octoba 29

Image copyrightGETTY IMAGES
Bingwa wa masumbwi uzani mzito kutoka Uingereza Tyson Fury ameahirisha marejeo ya pambano lake na Wladimir Klitschko kwa mara ya pili kwasababu ''afya yake hairidhishi''.
Mapromota wake hawakufichua taarifa zaidi lakini wamesema " hali yake ni mbaya mno na haimruhusu kushiriki pambano hilo".
Fury, mwenye umri wa miaka 28, alimshinda Klitschko kutoka Ukraine kwa pointi katika pambano la kwanza mnamo Novemba mwaka jana.
Regeleo la pambano la awali lilipangwa Julai 9 katika uwanja wa Manchester Arena, na liliahirishwa hadi Juni baada ya Fury kuvunja fupa la kisigino chake.
Pambano jipya la maregeo kati ya mabondia hayo wawili liliangwa kufanyika Octoba 29.
"Tyson sasa inabidi afanyiwe matibabu anayohitaji ili aweze kupona kikamilifu," Hennessey Sports iliongeza.
"Tunaomba radhi kwa wote wanaohusika katika pambano hili na mashabiki wote wa masumbwi waliotazamia maregeo hayo. Ni wazi kuwa Tyson pia amehuzunishwa na hali ilivyo.
"Tutatoa taarifa zaidi katika muda unaofaa."

Friday, 23 September 2016

Conte: Nahitaji muda kuiboresha Chelsea.

Meneja wa Chelsea Antonio Conte mwenye umri wa miaka 47

Image copyrightGETTY IMAGES
Image captionMeneja wa Chelsea Conte aliwahi kushinda vikombe vitatu vya ligi alipokuwa na Juventus huko Italy
Meneja wa Chelsea Antonio Conte anasema anahitaji mda kuimarisha timu yake Chelsea kucheza anavyotaka yeye ili ipate matokeo bora, Je mashabiki watamuelewa?
''The Blues'' kama wanavyoitwa walikwenda sare na Swansea, wakapoteza mechi yao na Liverpool kabla kufanikiwa kuigonga Leicester City 4-2 kwenye mechi zao za hivi majuzi.
"Ni kawaida wakati unaanza kazi kwenye timu mpya unahitaji mda kutekeleza kile unachokusudia, nami naahidi tutaiboresha Chelsea'' Conte amenukuliwa kusema
Chelsea wanakutana na mahasimu Arsenal Jumamosi huku meneja wa Gunners Arsene Wenger akiwa anatafuta ushindi wa kusherehekea vizuri miaka 20, ifikapo 1 October, tangu kuwasimamia Wana-Emirates hao.
Kibarua cha Conte hata hivyo si rahisi- Msimu wa ligi uliopita Chelsea walibugia magoli 53.
"Hii inamaanisha lazima tufanye kazi ya ziada timu nzima tuboreshe upande wa ulinzi wetu, kwani iwapo unataka kuwa bingwa kisawasawa dawa ni kutofungwa mabao mengi hivyo."
Katika mechi ya Jumamosi dhidi ya Arsenal itabidi Conte atafute dawa ya dharura kwani hatakuwa na mchezaji anaemtegemea sana John Terry ambae anauguza jeraha.

Tuesday, 20 September 2016

Miamba ya ligi kuu ya England kushiriki katika EFL.

Jack Wilshere ameichezea Bournemouth ilipocharazwa 4-0 na Man City mwishoni mwa juma

Image captionJack Wilshere ameichezea Bournemouth ilipocharazwa 4-0 na Man City mwishoni mwa juma
Raundi ya 3 ya Kombe la Ligi , EFL CUP itachezwa Jumanne na Jumatano na kushirikisha kwa mara ya kwanza timu za ligi kuu ya England, zinazocheza Ulaya kwenye mashindano ya UEFA.
Mabingwa Watetezi Manchester City wao watacheza Ugenini Jumatano kuivaa Swansea City.
Mechi nyingine itachezwa Jumanne huko King Power Stadium kati ya Mabingwa wa England Leicester City na Chelsea.
Liverpool na Arsenal zipo Ugenini kwa kucheza na Timu za Derby County watacheza na Liverpool na Nottingham Forest kuivaa Arsenal.
Jumatano Man United wapo Ugenini kuivaa Northampton Town.
Jumanne Septemba 20
Bournemouth v Preston, Brighton v Reading, Derby v Liverpool, Everton v Norwich, Leeds v Blackburn, Leicester v Chelsea, Newcastle v Wolves, Nottm Forest v Arsenal
Jumatano Septemba 21
Fulham v Bristol City, Northampton v Man Utd, QPR v Sunderland, Southampton v Crystal Palace, Swansea v Man City, West Ham v Accrington, Stoke v Hull, Tottenham v Gillingham.

Saturday, 10 September 2016

Kama Neymar angehama FC Barcelona, angekuwa mchezaji anayelipwa zaidi.


September 9 2016  wakala wa mshambuliaji wa na nahodha wa timu ya taifa ya Brazilanayeichezea FC Barcelona Neymar, ameweka wazi kuwa staa huyo alikuwa ahame katika kipindi hiki cha usajili cha majira ya joto.
Wakala wa Neymar anayejulikana kwa jina la Wagner Ribeiro ameweka wazi kuwa staa huyo alikuwa ajiuge na vilabu vya Man United au Paris Saint Germain ya Ufaransa, kwani vilionesha dhamira ya wazi ya kuhitaji huduma ya staa huyo.
Wagner Ribeiro ameeleza kuwa kabla ya Neymar kuongeza mkataba wa miaka mitano wa kuitumikia FC Barcelona, alikuwa ajiunge na PSG au Man UnitedWagner Ribeiroameeleza kuwa PSG walikuwa wanataka kumlipa Neymar mshahara wa euro 770,000 kwa wiki ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 1.8.

Friday, 9 September 2016

Mourinho: Man City watakuwa hatari bila Sergio Aguero.

Sergio Aguero

Image copyrightGETTY IMAGES
Image captionAguero anatumikia marufuku kwa kumchezea visivyo Winston Reid wa West Ham
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema itakuwa vigumu kucheza dhidi ya Manchester City wakiwa bila Sergio Aguero Jumamosi.
Mshambuliaji huyo wa Argentina, 28, amepigwa marufuku kucheza mechi tatu baada ya kumgonga mchezaji wa West Ham kwa kiwiko cha mkono mechi ambayo City walishinda 3-1.
Aguero amefunga mabao matatu katika mechi tatu alizocheza Ligi ya Premia msimu huu lakini Mourinho anasema kutokuwepo kwake kuna maana kwamba City, chini ya Pep Guardiola hawataweza kutabirika.
"Akiwa hachezi, basi wana wachezaji wengine wengi wanaweza kutumia," amesema Mourinho.
"Inakuwa vigumu zaidi. Sergio Aguero akiwepo basi unajua atacheza, na unajua watajipanga vipi."
Mourinho amesema mmoja kati ya Kelechi Iheanacho, Raheem Sterling na David Silva anaweza kuchezeshwa kama 'nambari tisa bandia' kwenye debi hiyo Old Trafford.

Arsene Wenger: Sitaki Jack Wilshere ahame Arsenal.

Jack Wilshere

Image copyrightREX FEATURES
Image captionWilshere, amechezea Arsenal mechi zaidi ya 100
Arsene Wenger amesema matumaini yake ni kwamba kiungo wa kati Jack Wilshere, ambaye kwa sasa ametumwa Bournemouth kwa mkopo, atasalia Arsenal maisha yake ya uchezaji.
Wilshere, 24, ambaye huchezea timu ya taifa ya Uingereza, alienda Bournemouth kwa mkopo wa msimu mmoja.
Ni mmoja wa wachezaji waliokua kutoka chuo cha kustawisha wachezaji cha Arsenal na aliwachezea mechi yake ya kwanza 2008 akiwa na miaka 16.
Lakini alicheza mechi tatu pekee klabu hiyo msimu uliopita kutokana na majeraha.
"Yeye ni mchezaji stadi sana, hahitajiki kufanya jambo jingine kunionyesha uwezo wake," amesema Wenger.
"Binafsi, natumai atasalia hapa maisha yake yote ya uchezaji."
Wenger amesema walizungumza na mchezaji huyo.
Bournemouth watakutana na West Bromwich Albion Jumamosi na Wilshere anatarajiwa kucheza.

Saturday, 3 September 2016

Kauli za Mario Balotelli kwa waandishi wa habari baada ya kujiunga na Nice.


Usiku wa August 31 kuamkia September 1 ndio siku ambayo dirisha la usajili la majira ya joto barani Ulaya lilifungwa rasmi, kuna mengi yametokea ikiwemo kushuhudia mshambuliaji wa kimataifa wa Italia aliyekuwa anaichezea klabu ya Liverpool Mario Balotelli akitolewa bure.
Balotelli alitolewa bure kwenda katika klabu ya Nice ya Ufaransa iliyopo nafasi ya katika msimamo wa Ligi Kuu Ufaransa, baada ya kuwasili Nice ya Ufaransa waandishi wa habari kama kawaida walimuuliza maswali Mario Balotelli katika press conference, majibu ya Balotelli hayajatofautiana sana na utukutu wake.

Kauli za Mario Balotelli kwa waandishi wa habari baada ya kujiunga na Nice.


Usiku wa August 31 kuamkia September 1 ndio siku ambayo dirisha la usajili la majira ya joto barani Ulaya lilifungwa rasmi, kuna mengi yametokea ikiwemo kushuhudia mshambuliaji wa kimataifa wa Italia aliyekuwa anaichezea klabu ya Liverpool Mario Balotelli akitolewa bure.
Balotelli alitolewa bure kwenda katika klabu ya Nice ya Ufaransa iliyopo nafasi ya katika msimamo wa Ligi Kuu Ufaransa, baada ya kuwasili Nice ya Ufaransa waandishi wa habari kama kawaida walimuuliza maswali Mario Balotelli katika press conference, majibu ya Balotelli hayajatofautiana sana na utukutu wake.

Kauli za Mario Balotelli kwa waandishi wa habari baada ya kujiunga na Nice.


Usiku wa August 31 kuamkia September 1 ndio siku ambayo dirisha la usajili la majira ya joto barani Ulaya lilifungwa rasmi, kuna mengi yametokea ikiwemo kushuhudia mshambuliaji wa kimataifa wa Italia aliyekuwa anaichezea klabu ya Liverpool Mario Balotelli akitolewa bure.
Balotelli alitolewa bure kwenda katika klabu ya Nice ya Ufaransa iliyopo nafasi ya katika msimamo wa Ligi Kuu Ufaransa, baada ya kuwasili Nice ya Ufaransa waandishi wa habari kama kawaida walimuuliza maswali Mario Balotelli katika press conference, majibu ya Balotelli hayajatofautiana sana na utukutu wake.