Mshambuliaji wa Crystal Palace Jonathan Benteke, atasalia nje ya uwanja kwa miezi mitatu hadi minne kutokana na jeraha la goti.
Mbelgiji huyo mwenye umri wa miaka 21 , kakake mdogo Christian Benteke, ameshiriki mechi moja klabu hiyo tangu alipojiunga nao rasmi mwezi Agosti.
Meneja Alan Pardew amesema habari kuhusiana na jeraha hilo zilikuwa za ''kukasirisha,'' kwa klabu hiyo na hata wachezaji.
Pardew, ambaye timu yake itacheza dhidi ya Everton katika mechi ya ligi ya Premia siku ya Ijumaa, alisema: '' Shida ya jeraha la goti ndiyo shida kuu.''
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT