Mambo ya kufahamu baada ya uzinduzi wa Phantom 6 na Phantom 6 Plus. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Thursday, 29 September 2016

Mambo ya kufahamu baada ya uzinduzi wa Phantom 6 na Phantom 6 Plus.


Kampuni ya simu Afrika Tecno Mobile imezindua simu mbili matata za Phantom 6 na Phantom 6 Plus katika tukio lililohudhuriwa na watu maarufu kibao katika Hotel ya Armani ambayo ipo katika jengo refu zaidi duniani ‘BurjKhalifa’ Dubai. Uzinduzi huo pia  umefanyika wakati kampuni ya Tecno inatimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake.
Wakizungumza katika hafla ya uzinduzi wa simu hizo, Mkuu wa Masoko wa Tecno  Vane Ni  na Naibu Kiongozi wa Masoko wa Tecno Nigeria Attai Oguche wamesema…….>>> ‘TECNO Phantom 6 inawapa watumiaji wa simu za mkononi utulivu bora pindi wanapotumia, kasi na kamera bora na nzuri ili kufurahia zaidi simu ya mkononi lakini pia imetuchukua takribani miaka 3 katika matengenezo yake na imehusisha zaidi ya wahandisi laki 5′
Baada ya uzinduzi huo Tecno Tanzania imetangaza kwamba Phantom 6 na Phantom 6+ zitaanza kupatikana rasmi kuanzia tarehe 8 October 2016 katika duka la Tecno lililopo City Mall Posta ambapo wateja wote watakaonunua Phantom 6 siku hiyo watapatiwa vifurushi vya zawadi na kutakuwa na zawadi kubwa nono.
Aidha wametangaza  kwamba kuanzia Jumatatu October 3 mwaka huu wateja watajaza fomu maalum ili kuweka oda zao na watazawadiwa zawadi mbalimbali zikiwemo T-Shirts, mabegi, T-Band na Sefie stick siku ya kuanza mauzo hiyo tarehe 8 October. Kuhusu bei mtu wangu Tecno wameangalia hali halisi ya uchumi kwa sasa ambapo gharama itakuwa kati ya Tsh 500,000 – Tsh 600,000.

tza3
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT