bongo satellite.: Michezo-Duniani.
Breaking News
Loading...
Showing posts with label Michezo-Duniani.. Show all posts
Showing posts with label Michezo-Duniani.. Show all posts

Tuesday, 27 September 2016

Michuano ya vilabu bingwa Ulaya kuendelea.

Harry Kane

Image captionHarry Kane
Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane ataendelea kuuguza jeraha lake la kifundo cha mguu wakati ambapo timu yake inakabiliana na CSKA Moscow katika kombe la vilabu bingwa Ulaya siku ya Jumanne.
Tottenham itamkosa beki wake wa kushoto Danny Rose na kiungo wa kati Eric Dier,Mousa Dembele na Moussa Sissoko.
Katika mechi nyengine itakayohusisha klabu ya Uingereza,kipa wa Leicester Kasper Schmeichel huenda akarudi kuichezea klabu yake katika mchuano wa kwanza wa kombe la vilabu bingwa Ulaya kwa klabu hiyo kushiriki nyumbani wakati watakapoikaribisha klabu ya Ureno Porto.
Schmeichel amekuwa nje kwa mechi tatu tangu Leicester iishinde Cub Brugge katika mechi yao ya ufunguzi ya Kundi G.
Mechi nyengine zitakazochezwa hii leo ni:
CSK vs Tottenham
Leicester vs FC Porto
Monaco vs Bayer Levkn
Bor Dortmd vs Real Madrid
Sporting vs Legia War
FC Copenhagen vs Club Brugge
Dinamo Zagreb vs Juventus
Sevilla vs Lyon
bbc.

Monday, 26 September 2016

PICHA 10: Ijue top 10 ya wacheza mieleka matajiri zaidi duniani.


  list ya wachezaji mieleka 10 matajiri zaidi duniani.
Na hii ndio list ya wacheza mieleka 10 matajiri Duniani

10. MARK CALAWAY A.K.A THE UNDERTAKER ($16 MILLION ZAIDI YA TSH BIL 34)

1200-1024x683

9. SHAWN MICHAELS ($17 MILLION ZAIDI YA TSH BIL 37)

sue411_shawn_michaels-1024x576

8. CHRIS JERICHO ($18 MILLION ZAIDI YA TSH BIL 39)

063_raw_09012014mm_0325-2538468490-1424615886-1024x576

7. PAUL RANDALL WIGHT A.K.A BIG SHOW ($19 MILLION ZAIDI YA TSH BIL 41)

7

6. KURT ANGLE ($20 MILLION ZAIDI YA TSH BIL 43)

6

5. PAUL LEVESQUE A.K.A TRIPLE H ($25 MILLION ZAIDI YA TSH BIL 54)

5

4. JOHN CENA ($35 MILLION ZAIDI YA TSH BIL 76)

4

3. STEVE AUSTIN A.K.A STONE COLD ($45 MILLION ZAIDI YA TSH BIL 98)

3

2. HULK HOGAN ($100 MILLION ZAIDI YA TSH BIL 217)

2

1. DWAYNE JOHNSON A.K.A THE ROCK ($250 MILLION ZAIDI YA TSH BIL 544)

1
Millard Ayo.

Tyson huenda asipigane tena.

Bingwa wa masumbwi katika uzani mzito duniani Tyson Fury

Image captionBingwa wa masumbwi katika uzani mzito duniani Tyson Fury
Bingwa wa uzani mzito duniani Tyson Fury huenda asipigane tena ,kulingana na afisa wa mauzo katika ndondi ya kulipwa nchini Uingereza.
Fury mwenye umri wa miaka 28 amejiondoa katika pigano la marudiano kati yake na Wladimir Klitschko lililotarajiwa kufanyika Oktoba 29 kutokana na matatizo ya kiafya .
Muingereza huyo ambaye hajapigana tangu kumshinda Klitschko mnamo mwezi Novemba mwaka uliopita aliahirisha mechi hiyo mnamo mwezi Juni.
"Fury atapokonywa mataji yake na baada ya makabiiano ya kisheria mahakamani, atasema ''sitaki tena'' ,alisema Hearn.
''Itakuwa makabiliano makubwa na itachukua mwaka mmoja kutatua.Najua kuna maswala nyeti kuhusu afya yake lakini hii ni biashara''.
''Bodi zinazosimamia mataji hayo zimetoshekwa.Ukanda wa uzani mzito duniani ni biashara yao kubwa na hawajapata fedha zozote kutokana na ukanda huo mwaka mmoja sasa''.
Bbc.

Wednesday, 7 September 2016

Guardiola hamuhitaji ila vilabu viwili vikubwa EPL vinahusishwa kumuhitaji Yaya Toure.


Ukizungumzia headlines za usajili wa soka barani Ulaya kwa vilabu na wachezaji bado wamekuwa wakihusishwa kwenda katika vilabu mbalimbali na wengine kuongeza mikataba, ila ishu ipo kwa kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast anayeichezea Man City Yaya Toure kuwa hataenda klabu gani baada ya Guardiola kuonesha kutomuhitaji.
Tayari wakala wa Yaya Toure ameshathibitisha kuwa kiungo huyo ataondoka Man City mwezi January, hiyo inatokana na kutoorodheshwa na Guardiola katika kikosi cha wachezaji 21 watakaocheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2016/2017.
Headlines zilizoandikwa na Sky Sports kwa sasa ni kuwa Man United na Arsenal wameonesha nia ya kumuhitaji Toure na tayari walikuwa wamehusishwa kuzungumza na wakala wake kabla ya muda mchache kusema kuwa uhamisho wa nyota huyo kujiunga na vilabu hivyo bado ni mgumu.
Millard Ayo.

Tyson Fury kuzipiga tena na Klitschko.

Tyson Fury kushoto akimenyana na Wladmir Klitschko katika pigano lao la kwanza

Image captionTyson Fury kushoto akimenyana na Wladmir Klitschko katika pigano lao la kwanza
Pigano la marudiano kati ya bingwa wa ndondi katika uzani mzito duniani Tyson Fury's dhidi ya Wladmir Klitscko limethibitishwa kufanyika Octoba 29.
Bingwa wa Uingereza Fury mwenye umri wa miaka 28 alijishindia mataji ya WBO,WBA, na IBF kutoka kwa raia huyo wa Ukraine mwenye umri wa miaka 40 mnamo mwezi Novemba mwaka 2015,lakini akajiondoa katika pigano la marudio lililopangwa kufanyika mwezi Julai kutokana na jeraha la kifundo cha mguu.
Pigano hilo litafanyika katika ukumbi wa Manchester.
''Ninafurahi kwamba tutapigana tena.sasa tutalenga kuwapatia mashabiki kile walichokitaka'',alisema meneja wa Tyson Fury na mjombake Peter.
Klitschko alikuwa hajawahi kushindwa kwa miaka 11 na alimiliki mikanda hiyo tangu mwaka 2006 kabla ya kupoteza kwa Fury mjini Dusseldorf kwa wingi wa pointi.
bbc.

Tuesday, 6 September 2016

PICHA: Kiatu ADIDAS walichomtengenezea Pogba kwa ajili ya mechi na Man City.


Kampuni ya vifaa vya michezo ya Ujerumani ADIDAS tayari imetengeneza kiatu maalum atachovaa mchezaji aliyeuzwa kwa gharama ya juu zaidi katika rekodi ya usajili Paul Pogba kwa ajili ya mchezo wa derby utakaochezwa weekende.
ADIDAS ambao wana mkataba wa udhamini na Paul Pogba wametengeneza kiatu maalum kwa ajili wa nyota huyo wa Ufaransa aliyejiunga na Man United akitokea Juventus.

Saturday, 13 August 2016

Januzaj ajiunga na Sunderland kwa mkopo kutoka Man Utd.

Adnan Januzaj

Image copyrightGETTY IMAGES
Image captionAdnan Januzaj
Winga wa Manchester United Adnan Januzaj, amejiunga na sunderland kwa mkopo msimu huu wa 2016/17.
Uhamisho huo umemuunganisha na meneja wake wa zamani David Moyes pamoja na wachezaji weza Donald Love na Paddy McNair aliyejiunga na timu hiyo kwa kitita cha pauni milioni 5.5 wiki hii.
Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Ubeligiji, Januzaj, alikuwa anataka kutoka Old Trafford kabisa lakini klabu hiyo ya United iliamua kumkabidhi kwa klabu hiyo kwa mkopo.
Adnan Januzaj (kulia)
Image captionAdnan Januzaj (kulia)
Januzaj alifunga mabao matano katika mechi 63 alizoshiriki kwenye klabu ya United.
Mkataba wake na Manchester United utamalika mwaka 2018.
Winga huyo alijiunga na timu ya Borussia Dortmund msimu uliopita kwa mkopo wa miezi minne, lakini alishiriki katika mechi 12 kabla ya kurudi katika timu yake ya Manchester United.

Leicester City wachapwa 2-1 na Hull mechi ya kufungua msimu.

Wachezaji wa Hull

Image copyrightREUTERS
Image captionSnodgrass amefunga bao la ushindi dakika ya 55
Mabingwa watetezi wa Ligi ya England Leicester City wameanza msimu wa 2016/17 kwa kuchapwa ugenini na Hull City.
Leicester wamechapwa 2-1, mabao ya Hull yakifungwa na Adama Diomande (46+2') na Robert Snodgrass (55').
Bao la kufutia machozi ya Leicester City limefungwa na Riyad Mahrez kupitia mkwaju wa penalti dakika ya 47.
Leicester CityImage copyrightPA
Leicester City ndio mabingwa wa kwanza watetezi kushindwa mechi ya kwanza ya msimu uliofuata kutwaa ubingwa enzi ya Ligi ya Premia.

Matokeo ya mechi zilizochezwa Jumamosi

  • Hull 2-1 Leicester
  • Burnley 0-1 Swansea
  • Crystal Palace 0-1 West Brom
  • Everton 1-1 Tottenham
  • Middlesbrough 1-1 Stoke
  • Southampton 1-1 Watford

Wednesday, 10 August 2016

Ranieri aongeza mkataba Leicester City.

Claudio Ranieri

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya England Leicester City wamemuongezea mkataba wa miaka minne kocha wao Claudio Ranieri.
Mkataba huo mpya utamuweka kocha huyo raia wa Italia, mwenye umri wa miaka 64, kwa mabingwa hao mpaka mwezi Juni, mwaka 2020.
Ranieri anaungana na wachezaji Kasper Schmeichel, Wes Morgan na Jamie Vardy waliongeza mikataba ya muda mrefu katika klabu hiyo.
Makamu mwenyekiti wa timu hiyo Aiyawatt Srivaddhanaprabha, amesema kocha huyo yuko katika mpango wa muda mrefu wa timu hiyo kwa kuwa na ujuzi mkubwa na uzoefu.
Katika msimu wake wa kwanza kocha huyo aliwapa ubingwa timu hiyo Ranieri amewahi kuvifundisha vilabu vikubwa kama Chelsea, Juventus, Inter Milan na AS Roma.

Hatma ya Wenger Arsenal yategemea msimu huu.

Arsene Wenger

Image copyrightGETTY IMAGES
Image captionKandarasi ya Arsene Wenger itakamilika mwisho wa msimu huu
Meneja wa klabu ya Arsenal ya Uingereza, Arsene Wenger ameiambia BBC kuwa hatma yake katika klabu hiyo ya Emirates inategemea jinsi matokeo ya klabu hiyo msimu huu yatakavyokuwa.
''Mkataba wangu utakamilika Juni mwakani kwa hivyo nitakachofanya baada ya hapo itategemea na matokeo ya msimu huu'' alisema Wenger.
Raia huyo wa Ufaransa 66, aliajiriwa mwezi Septemba 1996 kuiongoza klabu hiyo.
Mkataba wake wa sasa utakamilika mwishoni mwa mwezi juni mwaka ujao.
Arsenal haijashinda taji la ligi kuu ya Uingereza tangu mwaka wa 2004 jambo ambalo limechochea uhasama dhidi ya Wenger haswa kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo.
Awali wenger alikuwa amehusishwa na wadhfa wa kocha wa timu ya Uingereza lakini Sam Allardyce akachaguliwa kuchukua pahala pake Roy Hodgson.

Tuesday, 9 August 2016

Sahau kuhusu Chelsea, Ufaransa wameandika klabu anayotaka kujiunga nayo Mahrez.

Bado headlines za usajili zinazidi kuchukua nafasi barani Ulaya, tayari tumeshuhudia mastaa kadhaa wakivihama vilabu vyao na kujiunga na vingine, kwa upande wa Englandjina la winga wa kiwamataifa wa Algeria anayeichezea klabu ya Leicester City  Riyad Mahrez limerudi tena kwenye headlines za usajili.
Ufaransa kupitia mtandao wa EuroSport wameandika stori kuwa winga huyo amesema anataka kujiunga na Arsenal ya London na sio Chelsea, kwa mujibu wa EuroSportMahrez ana lengo la kujiunga na Arsenal ila hajataka kuweka wazi.
Licha ya mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha kutangaza wiki kadhaa kuwa Mahrez ataendelea kubakia King PowerEuroSport wamezidi kuzipa uzito headlines za staa huyo kuhama King Power na kujiunga na Arsenal.

Paul Pogba:Manchester United wamnunua kiungo wa ufaransa kwa euro 89m.

pogba

Image copyrightGETTY IMAGES
Image captionPogba amechezea timu ya taifa ya Ufaransa mechi 38
Paul Pogba amesema huu "ndio wakati bora zaidi wa kurejea Old Trafford" baada yake kukamilisha kuhamia Manchester United kwa kununuliwa £89m kutoka Juventus, ambayo ni rekodi mpya ya dunia.
Kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 23 amerejea miaka minne baada ya kuondoka United na kwenda Juventus kwa £1.5m mwaka 2012.
Pogba, ambaye ametia saini mkataba wa miaka mitano, ameongeza, "Hii ndiyo klabu bora kwangu kutimiza kila kitu ambacho kimekutumainia."
Meneja Jose Mourinho amesema mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa huenda akawa nguzo ya klabu hiyo kwa mwongo mmoja ujao.
United watalipa mabingwa hao wa Italia euro 105m kumchukua Pogba, pamoja na nyongeza euro 5m (£4.5m) ambayo ni bonasi kwa kutegemea mafanikio yake pamoja na gharama nyingine.
Paul Pogba
Bei yake imezidi ya mshambuliaji wa Wales Gareth Bale aliyenunuliwa £85m kuhamia Real Madrid kutoka Spurs mwaka 2013.
Pogba alijiunga na United mara ya kwanza kutoka kwa klabu ya Le Havre ya Ufaransa mwaka 2009 akiwa na miaka 16, na akawachezea mechi chache kabla ya mkataba wake kumalizika Julai 2012.
Amecheza Juventus 178 na kuwafungia mabao 34 na kuwasaidia kufika fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya 2015.
Klabu hiyo ya Serie A ilikuwa imeahidi kumpa mkataba mpya. Real Madrid nao pia walitaka kumnunua.
paul pogbaImage copyrightGETTY IMAGES

Wachezaji walionunuliwa ghali karibuni

  • 2013 - Gareth Bale £86m (Tottenham Hotspur hadi Real Madrid)
  • 2009 - Cristiano Ronaldo £80m (Manchester United hadi Real Madrid)
  • 2009 - Kaka £56m (AC Milan hadi Real Madrid)
  • 2001 - Zinedine Zidane £46m (Juventus hadi Real Madrid)
  • 2000 - Luis Figo £37m (Barcelona hadi Real Madrid)

Pogba asaini mkataba wa miaka mitano Man U.

Paul Pogba

Image copyrightGETTY IMAGES
Image captionPaul Pogba
Paul Pogba amesema kuwa ni muda muafaka kurejea Old Trafford baada ya uhamisho wake wa Paundi 89 ulioweka rekodi ya dunia kwenda Manchester United.
Kiungo huyo mwenye miaka 23 anarejea tena klabuni hapo baada ya miaka minne alipoelekea Juventus kwa ada ya uhamisho wa pauni 1.5 milioni mwaka 2012.
Pogba, ambaye amesaini mkataba wa miaka mitano ameongeza kuwa ''hii ni klabu sahihi kwangu kupata mafanikio ninayoyahitaji.''
Meneja wa Man U Jose Mourinho amesema Pogba atakuwa muhimili mkubwa wa klabu hiyo kwa kipindi kirefu kijacho.
United itailipa Juventus ambao ni mabingwa wa Italia Euro 105 milioni sambamba na Euro 5 milioni ikiwa hii ikitegemea kiwango chake kitakavyokuwa.
Pogba akiwa jijini ManchesterImage copyrightREX FEATURES
Image captionPogba akiwa jijini Manchester
Pogba aliyeisaidia Ufaransa wenyeji wa michuano ya Euro 2016 kufika fainali ameshinda taji la Serie A katika miaka yote minne ndani ya klabu yake.

Monday, 8 August 2016

ARSENAL YAICHAPA MAN CITY.

Theo Walcott

Image copyrightREUTERS
Image captionArsenal itakufungua msimu ujao dhidi ya Liverpool siku ya Jumapili
Arsenal ilitoka nyuma na kuichapa Manchester City mabao 3-2 katika mechi ya kirafiki kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya uingereza EPL juma lijalo.
Mechi hiyo ilikuwa ya mwisho ya kujipima nguvu kabla ya kipenga cha kuanza kwa msimu mpya wa EPL.
Sergio Aguero ndiye aliyefunga bao la kwanza katika mechi hiyo ilichezwa katika uwanja wa Gothenburg.
Hata hivyo Alex Iwobi, Theo Walcott na Chuba Akpom wakaifungia The Gunners.
Vijana wa kocha Pep Guardiola walijifurukuta na kufunga moja la kupunguza aibu kupitia kwa Kelechi Iheanacho.
Arsenal wakishabikia ushindi dhidi ya Man CityImage copyrightREUTERS
Image captionArsenal wakishabikia ushindi dhidi ya Man City
Licha ya ushindi huo kocha wa Arsenal alisalia akijikuna kichwa baada ya Gabriel kuondolewa uwanjani kwa machela akiwa amejeruhiwa.
Wakati huo huo vibonde wao katika ligi kuu ya Uingereza Chelsea hawakuwa na afueni kwani pia wao walimpoteza John Terry aliyejeruhiwa katika mechi ya kirafiki dhidi ya Werder Bremen.
The Blues waliibuka washindi kwa mabao 4-2.
Katika mechi nyingine Liverpool iliambulia kichapo cha 4-0 mikononi mwa Mainz siku moja tu baada ya kuiduwaza Barcelona kwa kichapo sawa na hicho.