Guardiola hamuhitaji ila vilabu viwili vikubwa EPL vinahusishwa kumuhitaji Yaya Toure. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Wednesday, 7 September 2016

Guardiola hamuhitaji ila vilabu viwili vikubwa EPL vinahusishwa kumuhitaji Yaya Toure.


Ukizungumzia headlines za usajili wa soka barani Ulaya kwa vilabu na wachezaji bado wamekuwa wakihusishwa kwenda katika vilabu mbalimbali na wengine kuongeza mikataba, ila ishu ipo kwa kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast anayeichezea Man City Yaya Toure kuwa hataenda klabu gani baada ya Guardiola kuonesha kutomuhitaji.
Tayari wakala wa Yaya Toure ameshathibitisha kuwa kiungo huyo ataondoka Man City mwezi January, hiyo inatokana na kutoorodheshwa na Guardiola katika kikosi cha wachezaji 21 watakaocheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2016/2017.
Headlines zilizoandikwa na Sky Sports kwa sasa ni kuwa Man United na Arsenal wameonesha nia ya kumuhitaji Toure na tayari walikuwa wamehusishwa kuzungumza na wakala wake kabla ya muda mchache kusema kuwa uhamisho wa nyota huyo kujiunga na vilabu hivyo bado ni mgumu.
Millard Ayo.
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT