Pwani. Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako amesema ili Tanzania iwe miongoni mwa nchi zenye ushindani kwenye elimu duniani, juhudi zaidi zinahitajika kukuza na kusimamia kiwango chake.
Profesa Ndalichako alitoa kauli hiyo kwenye sherehe za kufunga mafunzo ya awali ya vijana wanaojitolea kwa mujibu wa Sheria, Operesheni Magufuli kundi la saba kutoka Kambi ya Ruvu JKT, Kibaha mkoani Pwani.
Alisema miongoni mwa mambo yanayopaswa kupigwa vita ili kufanikisha juhudi hizo ni wazazi kujiepusha kuwasaidia watoto wao kughushi vyeti, huku wakitambua hawana sifa. Alisema kitendo hicho kinalenga kuliangamiza Taifa na taaluma.
“Ni matumaini yangu kuwa vijana mnaomaliza mafunzo yenu leo mtakuwa viongozi wa kuihamasisha jamii, pia mabalozi wazuri wa kutambua umuhimu wa kuboresha elimu na kupiga vita vitendo vyote vinavyolenga kudumaza na kudumisha amani na uzalendo wa nchi yetu,” alisema.
Chanzo:Mwananchi.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT