YA ROHONI,SOMA HII ITAKUSAIDIA:MTAZAME MUNGU,WALA SIO MATATIZO UNAYOYAPITIA. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Thursday, 9 June 2016

YA ROHONI,SOMA HII ITAKUSAIDIA:MTAZAME MUNGU,WALA SIO MATATIZO UNAYOYAPITIA.

UJUMBE WA JANA USIKU,USOME MPAKA MWISHO,
MTAZAME MUNGU,WALA SIO MATATIZO UNAYOYAPITIA.
BWANA YESU KRISTO ASIFIWE MPENDWA,
Ujumbe huu ukaja wakati najiandaa kuondoka mtandaoni,nikamsikiliza Roho wa Mungu,akaniambia andika hicho ninachokushuhudia itamponya mtu,
Ni kwamba wakati mwingi tunapenda kuyalalamikia matatizo au changamoto tunazokumbana nazo katika maisha,suala la kwanza la kulijua na kulitambua,fahamu ya kuwa Wanadamu au wewe binafsi hatupo/haupo tena Bustani ya Edeni ile ambayo Mungu kitambo alitupa(palipokuwa na starehe,tuitarajie Edeni mpya tutendapo matendo mema na kuzitii,kuzishika amri zake Mungu bila kuzimia roho hadi hapo Mwokozi wetu YESU KRISTO atakaporejea kutupeleka maskani kwa Baba yake alikotuahidi kupitia wanafunzi wake kuwa naenda kuwaandalia makao,maana hapo atakapo kuwa Yeye nasi tutakuwepo,)kwa masharti ya maagizo yake,lakini tamaa ilimponza mwanadamu kwa kukubali ushawishi,na tangia siku hiyo ule uwepo wa Mungu kwa 100% ukaondoka,eneo pekee ambalo tusingeona shida zozote,ndipo tulipoondolewa kwa sharti la mwanaume kula kwa jasho,na mwanamke kuzaa kwa uchungu,ndiyo maana mambo mengine tunajaribu kutumia sayansi ila bado hayawezi kupindua matamshi ya Mungu Aliye Hai.
Unakuwa unajikita katika kuliwaza sana tatizo unalo kumbana nalo,jangwa unalopitia,na mengi uyaonayo mbeleni,wana wa Israeli katika ukombozi kutoka Misri hata ile nchi ya ahadi Kanaani,walikumbana na mengi,utumwa,bahari,jangwa(na Mungu aliwanywesha na kuwalisha kwenye jangwa),mto,ukuta wa Yeriko,wafalme wa nchi ile ya ahadi,pamoja na kuongozwa na wingu mchana na moto usiku bado hawakuamini kuwa Mungu alikuwa nao,pamoja na Yeye kuwaambatanishia miujiza ila Yeye alitimiza ahadi yake aliyomuahidi Ibrahimu,na hatimaye wana wa Israeli waliweza kumiliki nchi ya ahadi(Kanaani).
Pia nawe mpendwa katika Bwana majira haya napenda kukutia nguvu na ujasiri kuwa Mungu anakutazama na kukusikiliza kwa yote umuombayo katika safari yako maishani,yapaswa wewe kudumu katika kumsikiliza Yeye,kuzitii amri na sheria zake kwa kuzifanya,milango unayoona imefunga,Yeye ana njia nyingi za kuzifungua usonge mbele,WATUMISHI WA MUNGU WOTE WALIOKUMBANA NA MATATIZO AU CHANGAMOTO MAISHANI ALIWAPA MILANGO YA KUTOKEA,nawe pia Yuko Yeye ambaye Yuko ili kukupatia mlango wa kutokea,kuelekeza maombi yako juu na kumtazama Yeye pekee,Mungu anajua hatma ya maisha yako,endelea kutenda mema na kuyashika maagizo yake,huku ukiendelea kupambana kwa ajili ya kile ukiaminicho kuwa ndiyo ndoto yako hapa Duniani,ukiutanguliza kwanza ufalme wa Mungu,MATHAYO 6:33.
Tazama JUU usiyaogope matatizo yaendee kwa ujasiri ukiwa umeongea na Mungu kwanza,Mtume Petro alipokuwa hajatazama juu kumuangalia Yesu Krsito apate kutembea juu ya maji alizama,hivyo nawe usikubali kutishwa na yale uyapitiayo,mtazame MUNGU PEKEE,TAZAMA JUU MAANA NDIKO KUNA MAELEKEZO YA KUFANIKIWA KATIKA KUYASHINDA HAYO UNAYO KUMBANA NAYO,MUNGU HUGAWA NGUVU ZA KUPATIA UTAJIRI UKIYATII MAAGIZO YAKE NA KUISKIA SAUTI YAKE,MAANA YA NGUVU YA UTAJIRI NI KWAMBA HUGAWA AFYA NJEMA,NA AKISHAKUPA NGUVU(AFYA),USIPO YAOGOPA MATATIZO MAANA HAYANA BUDI KUJA UTAFANIKIWA.
Mungu Aliye Hai na akuwezeshe kutazama juu kuliko na tumaini na uhakika wa kuyashinda yote.
YOTE YAWEZEKANA KWA IMANI,MAANA NI KUWA NA UHAKIKA NA MAMBO YATARAJIWAYO YASIYOONEKANA.
Namshukuru Mungu kupitia Roho Wake aliyenizuia kuondoka bila kuandika haya.
UBARIKIWE SANA NA MUNGU.
Shalom,Shalom(Amani,Amani).
@ Gideon Kiyyian Ole Kiyiapi .
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT