bongo satellite.: Elimu-Tanzania.
Breaking News
Loading...
Showing posts with label Elimu-Tanzania.. Show all posts
Showing posts with label Elimu-Tanzania.. Show all posts

Tuesday, 27 September 2016

MAELEKEZO KWA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA VYUO VYA UALIMU (JOINING INSTRUCTIONS) – 2016/2017.


 Maelekezo ya kujiunga na Vyuo vya Ualimu (Joining Instructions) – 2016

Friday, 23 September 2016

ORODHA YA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA UDOM MWAKA WA MASOMO 2016/2017.


Kupata majina ya wanafunzi walichaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dodoma ngazi ya Shahada, katika mwaka wa masomo 2016/2017, <<Bonyeza hapa>>

Mbunge wa Simanjiro James Ole Milya azindua madarasa manne ya shule ya msingi Emboreet,Simanjiro.

Mbunge wa Simanjiro James Ole Millya akishikana mikono na  Mwanamuziki wa nchini Marekani Kristie Cooter ishara ya  uzinduzi wa  madarasa manne katika shule hiyo yaliyojengwa kwa ufadhili wa shirika lisilokua la kiserikali la Wings of Kilimanjaro.Picha na Woinde Shizza
Mbunge wa Simanjiro James Ole Milya akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Emboreet mara baada ya kuzindua madarasa manne katika shule hiyo yaliyojengwa kwa ufadhili wa shirika lisilokua la kiserikali la Wings of Kilimanjaro.
Mbunge wa Simanjiro James Ole Millya akiteta jambo na Mwanamuziki wa nchini Marekani Kristie Cooter katika uzinduzi wa  madarasa manne katika shule hiyo yaliyojengwa kwa ufadhili wa shirika lisilokua la kiserikali la Wings of Kilimanjaro.PICHA NA WOINDE SHIZZA 

Tuesday, 6 September 2016

WIZARA YA ELIMU YAWAASA VIJANA KUTUMIA ELIMU KUJIAJIRI.

KLI1KLI1
Kaimu Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi  Bw. Nicholaus Bureta akizungumza wakati mkutano wa Vijana wa Afrika uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano  wa LAPF jana jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulijadili changamoto za ajira kwa vijana na suala la rushwa.
KLI2
KLI2Washiriki wa Mkutano wa Vijana wa Afrika wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mkutano wa Vijana wa Afrika uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano  wa LAPF jana jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulijadili changamoto za ajira kwa vijana na suala la rushwa
KLI3
KLI3Kaimu Kamishna wa Elimu Bw. Nicholaus Bureta akinyanyua juu nembo ya African Youth Leadership Transformation Summit (AYLTS) kuashiria uzinduzi wa nembo ya taasisi hiyo wakati wa hafla iliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
KLI4
KLI4Kaimu Kamishna wa Elimu Bw. Nicholaus Bureta akiwa kwenye picha ya pamoja na waandaaji wa Mkutano wa Vijana wa Afrika juu ya changamoto za ukosefu wa ajira na rushwa pamoja na suluhu za changamoto katika ukumbi wa Mikutano wa LAPF ulioko Millenium Tower jijini Dar es Salaam. (Picha Na: Lilian Lundo – MAELEZO)
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO Dar es Salaam
SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imewaasa vijana waliomaliza shule kuacha kujibetweka bali watumie elimu waliyoipata kujitafutia ajira ili kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira nchini.
Kauli hiyo imetolewa jana Jijini Dar es Salaam na Kaimu Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Nicholaus Bureta wakati wa ufunguzi wa mkutano wa vijana wa Afrika unaojadili changamoto zinazowakabili vijana katika nyanja mbalimbali za maendeleo.
Bureta alisema kuwa Serikali  inatoa elimu bora ili kuhakikisha vijana wanapata uwezo na maarifa yatakayowasaidia kujiajiri hata wasipopata nafasi za kuajiriwa katika taasisi na ofisi za umma pamoja na kuitumia elimu hiyo katika kupambana na vitendo vya rushwa.
“Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 inatutaka tuwe na watanzania walioelimika na wenye mtazamo chanya ambao utahakikisha jamii yetu inabadilika kufikia uchumi wa kati hivyo vijana msikae kusubiri ajira bali mjifunze jinsi ya kujiajiri kutokana na elimu mliyoipata mashuleni”, alisema Bureta.
Kwa upande wake Afisa Habari wa Umoja wa Mataifa (UN), Stellah Vuzo amewapongeza vijana hao kuamua kukusanyika kuchangia mawazo yao juu ya matatizo yanayowakabili kwani vijana wana nafasi kubwa ya kuhakikisha malengo mbalimbali yanatekelezeka.
Aidha, aliongeza kuwa Umoja wa Mataifa umemteua balozi kijana ambaye anashughulikia ajira za vijana hivyo amewaomba vijana walioshiriki katika mkutano huo kuyafikisha mawazo hayo kwa balozi huyo ili yaweze kupatiwa ufumbuzi.
Naye Mkuu wa Utafiti kutoka Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (PCCB), Daniel Pundu alisema kuwa tatizo la rushwa haliwezi kuisha endapo vijana hawatashirikishwa hivyo amewasisitiza vijana kushirikiana na Serikali kuchukua hatua za kupambana na rushwa ili kuhakikisha rushwa inaondoka.
“Tunajua kuwa vijana ndio nguvu kazi ya Taifa na ndio sababu tunawasisitiza kupambana na rushwa, kwa kulitambua hilo Serikali imeanzisha vilabu vya wapinga rushwa katika shule za sekondari na vyuo vikuu vikiwa na lengo la kuhakikisha vijana wanahusika kwenye mapambano hayo”, alisema Pundu.(P.T)
Mjengwa Blog.

Saturday, 3 September 2016

Ndalichako awafunda wahitimu JKT.


Pwani. Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako amesema ili Tanzania iwe miongoni mwa nchi zenye ushindani kwenye elimu duniani, juhudi zaidi zinahitajika kukuza na kusimamia kiwango chake.
Profesa Ndalichako alitoa kauli hiyo kwenye sherehe za kufunga mafunzo ya awali ya vijana wanaojitolea kwa mujibu wa Sheria, Operesheni Magufuli kundi la saba kutoka Kambi ya Ruvu JKT, Kibaha mkoani Pwani.
Alisema miongoni mwa mambo yanayopaswa kupigwa vita ili kufanikisha juhudi hizo ni    wazazi  kujiepusha kuwasaidia watoto wao kughushi vyeti, huku wakitambua hawana sifa. Alisema kitendo hicho kinalenga kuliangamiza Taifa na taaluma.
“Ni matumaini yangu kuwa vijana mnaomaliza mafunzo yenu leo mtakuwa viongozi wa kuihamasisha jamii, pia mabalozi wazuri wa kutambua umuhimu wa kuboresha elimu na kupiga vita vitendo vyote  vinavyolenga kudumaza na kudumisha amani na uzalendo wa nchi yetu,” alisema.
Chanzo:Mwananchi.


Sh225 mil zahudumia wanafunzi hewa.


Wanafunzi hewa waliobainika wilayani Kahama, wameisababishia hasara Serikali ya Sh225 milioni kwa kipindi cha miezi minane kuanzia Januari hadi Agosti.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkulu alisema kamati maalumu aliyounda imebaini uwapo wa wanafunzi hewa 29,000, ambao wamekuwa wakiisababishia hasara Serikali kila mwezi.
“Serikali ya Awamu ya Tano tangu iingie madarakani imekuwa ikituma fedha kila shule kwenye mpango wa elimu bure, lakini maofisa elimu, waratibu kata, walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari wamebuni mbinu za kula fedha hizo kwa kuweka wanafunzi hewa kwenye shule zao,” alisema Nkulu.
Alitoa siku tatu kwa kila halmashauri kuwasilisha takwimu sahihi za wanafunzi ambazo zitalingana na idadi aliyonayo iliyopatikana baada ya kamati ya uchunguzi.

Bodi ya Mikopo Kumwaga Fedha kwa Waombaji wote.

HESLB
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesema wale wote walioomba mkopo mwaka huu na kukidhi vigezo watapewa.
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru alisema hayo juzi mjini hapa wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti kwa watu watano waliorejesha mkopo wa elimu ya juu kwa mkupuo na kwa hiari.
Badru alisema idadi ya walioomba mkopo mwaka huu ni wanafunzi 88,000 ambao bodi itahakikisha wale wote waliokidhi vigezo, wanapatiwa fedha kwa ajili ya elimu ya juu.
Mkurugenzi huyo ambaye amehimiza walionufaika na mikopo kulipa madeni yao, alisema mwaka jana, wanafunzi waliokopeshwa ni 55,000.
Kuhusu waliopewa vyeti ikiwa ni hatua ya kuwatambua, ni pamoja na mfanyakazi wa VETA Shinyanga, Richard Jafu aliyerejesha kwa mkupuo Sh 14,749,950 na Francis Mwilafi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo aliyelipa Sh 15,115,200.
Wengine ni Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga aliyerejesha Sh 255,000; Profesa Peter Msoffe ambaye ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Dodoma (UDOM) aliyerejesha Sh 1,430,749.
Mwingine ni Mbunge wa Biharamulo, Oscar Mukasa ambaye kiasi alichorejesha hakikutajwa ingawa mkurugenzi mtendaji wa HESLB, alisema amerejesha kiasi kikubwa kwa mkupuo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wadau hao walisisitiza umuhimu wa wanufaika wa mikopo kuirejesha kwa hiari ili kuiwezesha bodi hiyo kukopesha wanafunzi wengine.
Mbunge wa Biharamulo, Mukasa alishauri bodi hiyo kuangalia uwezekano wa kurekebisha vigezo kwa lengo la kuwawezesha wanafunzi watokao maeneo ya pembezoni kunufaika na mikopo hiyo ya elimu. Kwa upande wake, Mbunge wa Vwawa, Hasunga alisisitiza wabunge wanaodaiwa warejeshe mkopo kwa mkupuo.

Waziri Mkuu aitaka Wizara ya Elimu kuongeza wataalamu wa Afya nchini.


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi iweke mpango maalumu wa kuongeza wataalamu zaidi katika sekta ya afya ndani ya nchi ili kuipunguzia Serikali gharama za kusomesha wataalam hao nje ya nchi.
Ametoa agizo hilo Ijumaa, Septemba 2, 2016  wakati alipokagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Kampasi ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya na Sayansi ya Tiba Muhimbili (MUHAS) na Ujenzi wa Kituo cha Tiba cha Kimataifa cha Muhimbili katika eneo la Mloganzila.
Amesema Serikali zilizotangulia zimefanya kazi kubwa na nchi imefikia hatua nzuri ya kuongeza wataalam ndani ya nchi ambao watakwenda kutatua changamoto ya upungufu wa madaktari bingwa kwenye hospitali za mikoa na wilaya.
Waziri Mkuu amesema ujenzi wa kituo hicho cha tiba cha kimataifa pia utawapunguzia wananchi adha ya kutafuta fedha za kwenda kupata matibabu nje ya nchi. Tayari upasuaji mkubwa wa magonjwa ya moyo umeanza kufanyika nchini.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Bw. Humphrey Polepole awasake watu wote waliohusika na wizi wa lita 1,000 za mafuta ya kuendeshea mitambo katika karakana ya mkandarasi anayejenga Kampasi hiyo.
“Wafanyakazi waache wizi. Lita 1,000 zinaondokaje katika karakana ya mkandarasi? Hii kampuni inayolinda kama imeshindwa kazi iondolewe na Mkuu wa wilaya usimhurumie mwizi,” amesisitiza.
Kwa upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako amesema kukamilika kwa kampasi ya Mloganzila kutasaidia upatikanaji wa madaktari bingwa wengi nchini ambao watapunguza gharama za kupeleka wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.
Awali, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Ephata Kaaya alisema kukamilika kwa hospitali pamoja na kampasi yote ya chuo kutawezesha kupunguza kwa kiasi kikubwa uhaba wa wataalamu wa afya nchini.
Amesema hospitali hiyo itatumika kutoa huduma za afya za kitaalam zaidi kwa magonjwa mbalimbali, hivyo kupunguza idadi ya wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kwa matibabu. Pia itapunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Ujenzi wa mradi huo umegharimu Dola za Kimarekani milioni 61, ambapo Serikali imetoa Dola milioni 18 na Serikali ya Korea imetoa mkopo wa Dola milioni 43. Kukamilika kwa ujenzi wa kampasi hiyo ya Mloganzila kutawezesha chuo kuongeza idadi ya udahili wa wanafunzi wa fani ya afya kutoka 4,010 hadi 15,000.
Prof. Kaaya amesema mkataba wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa mradi huo ulisainiwa tarehe 12, Desemba, 2014 na ujenzi ulianza mwezi Julai, 2015 na unatarajiwa kukamilika Oktoba, 2016.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA PILI NA KUONGEZWA KWA MUDA WA KUFANYA MAOMBI KATIKA KOZI ZA CHETI NA DIPLOMA KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017


Image
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu wote walioomba kudahiliwa katika kozi za cheti na diploma na Umma kwa ujumla kuwa lilifunga dirisha la maombi mnamo tarehe 13 Agosti 2016 ili kuruhusu uteuzi wa awamu ya pili kwa waombaji wa kozi hizo. Uteuzi wa awamu ya pili kwa waombaji wa cheti na diploma ulitarajiwa kutangazwa tarehe 31 Agosti 2016 lakini kwa sababu zilizo nje wa uwezo wetu umesogezwa mbele mpaka tarehe 5 Septemba 2016.

Baraza pia linapenda kutoa taarifa  kuwa Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS) kwa waombaji wa cheti na diploma utafunguliwa tena tarehe 5 Septemba 2016 hadi tarehe 15 Septemba 2016 ili kujaza nafasi za udahili zitakazokuwa wazi baada ya uchaguzi wa awamu ya pili. Hatua hii itawezesha kuruhusu machaguo mapya kwa wale ambao hawakuchaguliwa katika kozi walizoomba pamoja na  kuruhusu waombaji wapya ambao kwa njia moja au nyingine hawakuomba udahili hapo awali.
Baraza linaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza kutokana na mabadiliko hayo.
Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji
NACTE
Tarehe: 02 September, 2016

Thursday, 1 September 2016

Bodi ya mikopo kikaangoni.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako 
Dodoma. Wabunge wameibana Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB) kwa kuongeza posho na kufikia jumla ya Sh1 bilioni katika kipindi kifupi kiasi ambacho hakilingani na kazi wanayoifanya.
Kwa kipindi kirefu, bodi hiyo imekuwa ikitupiwa lawama kwa kuchelewesha mikopo, kushindwa kukusanya fedha za wanafunzi waliokopa na kutoa mikopo kwa wanafunzi hewa.
Hivi karibuni, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alisema bodi hiyo imetoa fedha za kujikimu na mafunzo kwa vitendo kwa zaidi ya wanafunzi hewa 1,000.
Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa HELSB, Abdul-Razaq Badru alijitetea mbele ya kamati hiyo akisema ni mgeni katika bodi hiyo na kwamba, wanaweka mikakati mizuri ya kurekebisha mambo hayo ili kuhakikisha inafanya kazi kwa weledi zaidi.
Wakizungumza katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) cha kukagua Ripoti ya Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka wa fedha 2014/15 ya bodi hiyo, wabunge hao walisikitishwa na kitendo cha bodi hiyo kushindwa kukusanya zaidi ya Sh3 trilioni walizowakopesha wanafunzi mbalimbali tangu ianze kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
Mwananchi.

Mpya: Waliochaguliwa kujiunga Kidato cha Tano 2016 Awamu Ya Pili.

emblem
OR-TAMISEMI imetangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya Pili (Second Selection) kwa mwaka 2016. Jumla ya wanafunzi 3,918 wakiwemo wasichana 2,413 na wavulana 1,505 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili kwa ajili ya kujaza nafasi zilizoachwa wazi na wanafunzi ambao hawakuripoti awamu ya kwanza.
Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 1,864 wakiwemo wasichana 1,099 na wavulana 765 sawa na asilimia 47.58 watajiunga na masomo ya Sayansi na Hisabati; na wanafunzi 2,054 wakiwemo wasichana 1,314 na wavulana 740 sawa na asilimia 52.42 wamechaguliwa kusoma masomo ya Sanaa na Biashara.
Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili mwaka 2015 wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti kwa zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya tangazo hili atakuwa amepoteza nafasi hii.
Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili mwaka 2016 inapatikana kwenye tovuti ya OR-TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz
Imetolewa na Katibu Mkuu,
OR-TAMISEMI
by Kurasa Mpya.

Tuesday, 30 August 2016

Tahadhari dhidi ya Taarifa za uongo kuhusu kutangazwa kwa Orodha ya wanafunzi waliodahiliwa kwa mwaka wa masomo 2016/2017.


tcu new

Friday, 19 August 2016

WANAFUNZI WA CHUO CHA UDOM WALIOPANGWA MAFUNZO YA UALIMU CHETI MTWARA-KAWAIDA 2016/17.


WANAFUNZI WA CHUO CHA UDOM WALIOPANGWA MAFUNZO YA UALIMU CHETI MTWARA-KAWAIDA 2016/17
KUTAZAMA MAJINA YA KAWAIDA <<BOFYA HAPA>>
KUONA MAJINA KWA PDF <<BOFYA HAPA>> 
JOINING INSTUCTIONS <<BOFYA HAPA>>
source: moe.go.tz

Thursday, 18 August 2016

MAJALIWA APOKEA MADAWATI TOKA KWA BALOZI WA KUWAIT NCHINI.

kuweit
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al Najem wakiwa wamekalia madawati mawili kati ya 50 yaliyotolewa na Kuwait na kukabidhiwa kwake na balozi huyo jijini Dar es salaam Agosti 17, 2016.. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea msaada wa sh. milioni 12 kutoka mashirika ya misaada ya Kuwait kwa ajili ya kununulia madawati ili kupunguza tatizo hilo nchini. Pia amepokea madawati 100 kutoka ubalozi wa Kuwait na taasisi ya Direct Aid ya nchi hiyo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo (Jumatano, Agosti 17, 2016), Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Bw. Jasem Al Najem amesema msaada huo ni michango kutoka mashirika ya misaada ya nchi yake ambayo yanatoa huduma mbalimbali hapa nchini.
“Tumejipanga kukamilisha ahadi ya madawati 600, tunaendelea kuwasiliana na wenzetu wa Kuwait Fund, na mashirika mengine. Kwa sasa tunachangia madawati, baadaye tutakwenda kwenye ujenzi wa madarasa, hata ikibidi tutaenda kwenye ujenzi wa shule,” alisema.
Balozi Najem amesema wanatoa misaada hiyo ili kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Dkt. John Magufuli za kutaka wanafunzi wote wakae kwenye madawati.
Akitoa shukrani mara baada ya kupokea msaada huo, Waziri Mkuu alimshukuru Balozi wa Kuwait kwa moyo wao wa kujitolea ikizingatia kuwa ni wiki tatu tu zilizopita alikwishatoa msaada mwingine wa madawati kwenye shule ya msingi Chamazi, wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.
Aliyashukuru pia mashirika ya misaada kupitia Ubalozi huo, ambao wametoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa madawati. Ametoa wito kwa mabalozi wengine, sekta binafsi na wadau wa maendeleo watoe michango zaidi ili yapatikane madawati ya kutosha.
Mashirika yaliyotoa michango hiyo ni African Relief Organisation (hundi ya sh. milioni 6), Al Furqaan Islamic Centre (hundi ya sh. milioni 6), Taasisi ya Direct Aid (madawati 50 ya shule za Msingi) na ubalozi wa Kuwait (madawati 50 ya shule za sekondari). (P.T)

Friday, 12 August 2016

TAHADHARI DHIDI YA MATAPELI KWA WAOMBAJI WA MIKOPO NA WADHAMINI WAO.


Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kuwatahadharisha waombaji wa mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2016/2017 na umma kwa ujumla kuwa imepokea taarifa kuwa kuna watu wasio waaminifu ambao si watumishi wa Bodi ambao huwapigia simu baadhi ya waombaji kwa lengo la kuwatapeli.
Taarifa hizo za kitapeli zimekuwa zikisambazwa katika siku za hivi karibuni kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii zikiwataka baadhi ya waombaji wa mikopo au wadhamini wao kutuma fedha (Tshs 39,000/-) kwa namba ya simu 0716463190 ili fomu zao za maombi ya mikopo zilizowasilishwa Bodi zirekebishwe kwa kuwa zimeonekana zina makosa na hivyo hawatapata mikopo.
Namba inayotumika kusambaza taarifa hiyo au kupiga simu kutoa taarifa hizo ni 0764640325 na mtu anayepiga anajitambulisha kwa jina la Charles Amos.
Bodi ya Mikopo inapenda kuwataarifu wadau wake wote, wakiwemo wale walioomba mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2016/2017 kuwa taarifa hizo si za kweli. Mtu huyo ni tapeli na si mtumishi wa Bodi ya Mikopo.
Iwapo waombaji watapigiwa simu na matapeli hao, watoe taarifa kwa vyombo vya dola kwa hatua zaidi.
Aidha, Bodi ya Mikopo inapenda kuwataarifu waombaji wa mikopo kuwa utaratibu wa Bodi kuwasiliana na waombaji wa mikopo ambao fomu zao za maombi hubainika kuwa na upungufu haujabadilika. Mara baada ya kazi ya ukaguzi wa fomu kukamilika, Bodi ya Mikopo itatoa taarifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari, ikiwemo tovuti hii ya Bodi na kuwaalika waombaji kufanya marekebisho.
Mwisho.
IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO,
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU,
IJUMAA, AGOSTI 12, 2016

Tuesday, 9 August 2016

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUONGEZWA KWA MUDA WA KUFANYA MAOMBI KATIKA KOZI ZA CHETI NA DIPLOMA KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017.


nacte
Baraza linapenda kuwaarifu wote walioomba kudahiliwa katika kozi za cheti na diploma na umma kwa ujumla kuwa muda wa nyongeza wa kutuma maombi kwa mwaka 2016/2017 umeongezwa hadi tarehe 13 Agosti 2016 ili kuruhusu ambao hawakukamilisha maombi yao kuyamaliza na ambao hawajafanikiwa kuomba kutuma maombi yao.

Baraza linaomba ifahamike kuwa vyuo na kozi zilizojaa hazitaonekana tena wakati wa maombi bali kozi zitakazoonekana ni zile zenye nafasi tu pia baraza linashauri waombaji wajipime na kuangali ushindani wa kozi ili kufanikisha kuchaguliwa kwao. Vyuo na kozi zilizo na nafasizimeainishwa hapa.

Baraza pia linapenda kuwaarifu waombaji waliofanya maombi kwenye vyuo vya Ualimu vya Serikali kuwa uteuzi kwenye vyuo hivyo unasubiri mwongozo wa Serikali na hivyo watafahamishwa punde uteuzi utakapokamilika. Waombaji wa vyuo hivi wanashauriwa kusubiri na kutokubadili machaguo yao hadi kutangazwa kwa uteuzi kwa vyuo vya Ualimu vya Serikali.

Baraza pia linapenda kuwataarifu waombaji waliokwisha chaguliwa kwenye awamu ya kwanza na wanataka kuomba uhamisho kutoka kozi ama chuo kimoja kwenda kingine wavute subira utaratibu utatolewa mara tu majibu ya waombaji wa awamu ya pili yatakapotolewa.

Aidha Baraza linapenda kuwafahamisha waombaji wa Shahada ya Kwanza (Bachelor Degree) waliofanya maombi kupitia mfumo wa pamoja wa udahili wa Baraza kuwa utaratibu wa kukamilisha maombi yao utatolewa baada ya mashauriano kati ya Baraza na Tume ya Vyuo Vikuu yatakapokamilika.

Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji
NACTE
Tarehe: 08th Agosti, 2016