Sasha Obama, binti wa Rais wa Marekani Barack Obama ameingia kwenye headline baada ya baadhi ya picha zake kusambaa mitandaoni zikimuonesha akiwa kwenye mgahawa mmoja amevalia sare ya hoteli akifanya kazi. Vyombo vya habari nchini Marekani vimeeleza kwamba ameamua kuacha ‘starehe’ za ikulu ya White House na kuanza kufanya kazi katika mgahawa huo.
Binti huyo mwenye umri wa miaka 15 ameanza kufanya kazi ya kuwahudumia wateja katika mgahawa mmoja ulioko Martha’s Vineyard, Massachusetts. Gazeti la Boston Herald limeripoti kuwa Sasha ambaye anatumia jina lake kamili, Natasha, aliambatana na maafisa sita wa ulinzi wa secret service siku yake ya kwanza kazini.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT