Mtanzania aliyesifiwa na Rais Obama arejea nchini, atoa neno kwa Serikali. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Saturday, 6 August 2016

Mtanzania aliyesifiwa na Rais Obama arejea nchini, atoa neno kwa Serikali.


Rais Barack Obama wa Marekani alikutana na vijana mbalimbali kutoka bara laAfrika ikiwa ni mpango wa serikali yake kila mwaka toka mwaka 2014 kukutana na vijana hao wanaohusika na kuivusha jamii kwenye ishu mbalimbali ikiwemo biashara na siasa.
Mwanaharakati wa haki za binadamu Mtanzania Mwanasheria Geline Fuko kutokea kwa Hellen Kijobisimba kwenye kituo cha sheria na haki za binadamu ni miongoni mwa vijana takribani 40 kutoka Tanzania ambao walishinda nafasi za kuja Marekani kwenye huo mpango wa Obama.
Nafasi hiyo ameipata baada ya kushiriki katika kutengeneza kanzidata ya katiba ambayo inatoa nafasi kwa watanzania kusoma mambo mbalimbali ya katiba, Usiku wa August 5 2016 Geline Fuko amerejea Tanzania na ametoa wito wake kwa serikali ya Tanzania kuhusu mchakato wa katiba mpya, Fuko amesema……
>>>’kilio cha watanzania kuhusiana na katiba bado kipo na mchakato tulishauanza ni vyema tukaumaliza katika namna ambayo kila mwananchi atapata nafasi ya kuridhika na namna mchakato utakavyokwenda, wito wangu kwa serikali mchakato wa katiba tunaomba muurudishe na muwakabidhi wanachi jukumu la kumalizia mchakato huu kwa namna wenyewe watakavyoona unafaa’ 
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT