Mke wa mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amekanusha madai kwamba huenda alivunja sheria za viza alipoanza kufanya kazi kama mwanamitindo jiji New York, Marekani.
Kupitia taarifa, Melania Trump amesema amekuwa akitii sheria na kanuni za uhamiaji "wakati wote"
Bi Trump hata hivyo bado hajafafanua alitumia viza ya aina gani alipopigwa picha za uanamitindo jijini New York mwaka 1995.
Amekuwa akisema alianza kufanya kazi kama mwanamitindo Marekani mwaka 1996, lakini picha zake za utupu zilizochapishwa na gazeti la udaku la New York zinaashiria kwamba huenda zilipigwa mwaka 1995 zikikusudiwa kutumiwa katika jarida moja la Ufaransa ambalo kwa sasa halichapishwi.
Mwandishi wa BBC jijini Washington Gary O'Donoghue anasema kasoro hiyo imeibua maswali kuhusu hali Melania wakati huo na iwapo alikuwa na kibali cha kufanya kazi Marekani.
Bw Trump amekuwa na msimamo mkali kuhusu wahamiaji haramu katika kampeni yake.
Kufikia sasa, maafisa wake wa kampeni wbado hajasema wazi Bi Trump alitumia viza gani na alipewa wakati gani.
Madai ya kwamba huenda mwanamke huyo alivunja sheria yamejiri katika wiki ambayo imekuwa na misukosuko kwa tajiri huyo kutoka New York.
Kuna taarifa za mgawanyiko mkubwa kutokea katika uongozi wa chama cha Republican kutokana na matamshi yenye utata ambayo yamekuwa yakitolewa na mgombea huyo.
Mmiliki wa mojawapo wa mawakala wa uanamitindo waliotumiwa na Melania, Paolo Zampolli, anasema alimdhamini Bi Trump na kumuwezesha kupata viza ya kufanyia kazi ya ngazi ya H1B mwaka 1996.
Melania amekuwa akisema alilazimika kurejea Slovenia, nchi yake ya kuzaliwa, mara kwa mara baada ya miezi kadha kufanya upya viza yake, jambo ambalo sana huhitajika kwa watu wanaotumia viza za kitalii au biashara na wala si za kufanya kazi.
bbc.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT