MANNY PACQUIAO KUKABILIANA NA JESSIE VARGAS NOVEMBA. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Friday, 5 August 2016

MANNY PACQUIAO KUKABILIANA NA JESSIE VARGAS NOVEMBA.

Manny Pacquiao

Image copyrightGETTY IMAGES
Image captionPacquiao ameshinda mapigano 58 kati ya 66
Mwanandondi Manny Pacquiao atarejea ulingoni mnamo tarehe 5 Novemba kukabiliana na bingwa wa dunia wa uzani wa welter Jessie Vargas kutoka Marekani
Pacquiao, 37, bingwa wa zamani wa dunia, ametangaza kwamba atarejea licha yake kutangaza kwamba angestaafu baada ya kumshinda Timothy Bradley mwezi Aprili.
Promota wake Bob Arum alisema mwezi uliopita kwamba mwanabondia huyo kutoka Ufilipino angepigana tena mwaka huu.
"Maisha ya kustaafu hayamfai Manny kwa sasa," meneja wa Pacquiao Michael Koncz aliambia gazeti la Los Angeles Times.
"Ndondi zimo kwenye damu yake."
Pacquiao na kundi lake watakutana 10 Agosti mjini Manila kuamua iwapo pambano hilo dhidi ya Vargas, 27, litaandaliwa Los Angeles au Dubai.
Pacquiao alishinda uchaguzi wa useneta Ufilipino mwezi Mei.
Vargas alitwaa ubingwa mwezi Machi baada ya kushinda raia mwenzake Sadam Ali.
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT