Gavana wa mji wa Instanbul nchini Uturuki amesema kuwa watu 11 wameuawa na wengine 36 kujeruhiwa kwenye mlipuko wa bomu uliolenga basi la polisi mapema hii leo.
Vasip Sahin amesema kuwa maafisa saba wa polisi ni miongoni mwa waathiriwa.
Kifaa kilichotumika kufanya shambulio hilo kinaaminika kuwa kililipuliwa na kifaa maalum mbali na eneo la tukio hilo, kulenga basi moja la polisi.
Hakuna kundi lolote ambalo limedai kuhusika na shambulio hilo, lakini mwandishi wa BBC mjini Instanbul anasema kuwa serikali inailaumu kundi la kigaidi la Kikurdi la PKK au mojawapo ya makundi yaliyojitenga na kundi hilo.
Februari na Machi mwaka huu wapiganaji hao wa Kikurdi walitekeleza mashambulio ya mabomu katika mji mkuu wa Ankara.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT