KUNA mtu mmoja aliwahi kusema, ukiona miti katika mitaa inayokupatia kivuli, usidhani ilijiotea yenyewe, isipokuwa mtu mmoja, miaka mingi nyuma, aliipanda. Labda yupo na anaiona miti hiyo inavyowasaidia wengi kupata kivuli.
Na hata matunda na vyakula tunavyokula, havikutokea tu leo, bali miezi kadhaa nyuma, watu waliingia shambani na kufanya yao. Ndiyo maana tunakwenda sokoni na madukani kila siku, kwa sababu tunajua kuna watu pia wanaamka asubuhi kuwahi kulima.
Hivi ndivyo ilivyo hata kwenye Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba ya Global Publishers. Inakupasa kuwekeza ili kuichukua zawadi hii kubwa hapo Juni 30, mwaka huu.
Siku zinazidi kuyoyoma na wiki zisizozidi tatu, Tanzania itamshuhudia mtu mwenye bahati ya pekee, atakayejishindia nyumba ya kisasa yenye thamani ya shilingi milioni 60 iliyopo jijini Dar es Salaam, ambayo itatolewa na Kampuni ya Global Publishers, inayochapisha Magazeti Pendwa ya Risasi, Amani, Uwazi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda na Championi.
Ni mjengo wa thamani kubwa, unaoweza kuwa wako kwa kununua kuponi inayopatikana kwenye magazeti yaliyotajwa hapo juu, kwa shilingi mia tano tu.
Katika kuhakikisha nyumba hiyo yenye samani ndani, Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho, aliikagua mwishoni mwa wiki iliyopita ili kuona kama mambo yanakwenda sawa na kukuta mafundi wakimalizia hatua za mwisho, kwani kwa sasa imekamilika kwa kiasi cha asilimia 99.
Lengo kubwa la ziara hiyo, ilikuwa ni kuangalia matengenezo madogomadogo ya mwisho ili kuhakikisha mjengo unakuwa kamili kwa kila kitu kabla ya Juni 30, mwaka huu wakati droo kubwa na ya mwisho itakapochezeshwa.
“Nyumba imekamilika kwa asilimia 99 kama unavyoona, kilichopo hapa ni vitu vidogovidogo tu vya mwisho ambavyo vitakamilika ndani ya wakati na mshindi ataipata ikiwa imekamilika kama tulivyoahidi,” alisema.
Kwa mujibu wa meneja Mrisho, nyumba hiyo ina chumba chenye kila kitu ndani (Master Bedroom), vyumba viwili vya kulala, chumba cha chakula (Dining room), chumba cha kupumzika (Sitting room), jiko, stoo na uwanja wa kutosha nje ya nyumba.
Wasomaji wa magazeti ya Global Publishers, wanatakiwa kukata kuponi iliyo ndani ya nakala za magazeti hayo na kuzituma kwa njia ya posta kwa kutumia anuani iliyooneshwa kwenye kuponi zao.
Njia zingine za kuhakikisha wanunuzi wa magazeti hayo yanayouzwa kwa shilingi 500 kila moja isipokuwa Ijumaa pekee ambalo sasa linauzwa shilingi 1000, wanafikisha kuponi zao sehemu husika ni kwa kuzipeleka kwa wakala wa magazeti hayo sehemu mbalimbali nchini au kuzifikisha katika ofisi za Global Publishers zilizopo Bamaga, Mwenge, jijini Dar es Salaam.
Kete ya bahati siku zote huwa haijulikani hadi kopo lifunuliwe. Bado hujachelewa kwa sababu huenda turufu ya ushindi unayo wewe unayesoma hapa muda huu. Nunua gazeti nyingi kadiri unavyoweza ili kupanua wigo wa ushindi.
Unapokuwa na kuponi 20 au 50 katika pipa moja kubwa, unakuwa na nafasi kubwa ya kushinda kuliko yule mwenye kuponi moja, ingawa dunia ya maajabu inakuambia wewe utakayekuwa na kuponi chache kwa vile ulichelewa kushiriki, unaweza kuibuka kuwa mshindi!
Nunua magazeti ya Global Publishers leo upate kumiliki nyumba hii ya kisasa kesho!
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT