Mfanyabiashara mwenye asili ya Uingereza Richard Alden amefikishwa Mahakamani akituhumiwa kuhusika na mauaji ya Grace Wangechi Kinyanjui ambaye alikuwa ni mke wake wa pili katika nyumba yake ya kifahari nchini Kenya, amefikishwa mahakamani baada ya polisi kukataa madai yake kuwa alijiua mwenyewe.
Mfanyabiashara huyo baada ya tukio alimpeleka Grace Wangechi Kinyanjui hospitali akidai kajipiga risasi mwenyewe na alifariki muda mfupi baadae kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata. Mtuhumiwa amefikishwa mahakamani na ataendelea kushikiliwa siku tano zaidi wakati polisi wakiendelea na uchunguzi.
Kamanda wa polisi Japheth Koome amesema wanandoa hao wamekuwa kwenye mahusiano na walikuwa wanaishi pamoja.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT