Waendesha mashtaka wamemtaka nyota wa Brazil na Barcelona Neymar kushtakiwa kwa udanganyifu wa fedha.
Waendesha mashtaka hao kutoka mahakama ya kukabiliana na uhalifu nchini Uhispania wanadai kwamba Neymar na babaake walificha thamani ya uhamisho wa mchezaji huyo kutoka Santos hadi Barcelona
Katika mahojiano ya awali Neymar amekana kufanya makosa yoyote.
Hazina moja ya uwekezaji ambayo ilimiliki asilimia 40 ya haki za Neymar inadai kwamba haikupata mgao wake kamili.
Barcelona inasema kwamba ililipa Yuro milioni 57 kumnunua Neymar mwaka 2013 huku wazazi wake Neymar da Silva Santos na Nadine Goncalves da Silva Santos akipata wakipokea Yuro milioni 40 na kilabu yake ya zamani Santos ikipokea Yuro milioni 17.
Lakini wachunguzi wanasema kuwa fedha hizo zilifika Yuro milioni 83 na Barcelona ilificha kiasi cha kitita hicho.
Klabu hiyo hata hivyo imekana kufanya makosa yoyote.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT