Hilarry Clinton uso kwa uso na Donald Trump
Hillary Clinton ameripotiwa kufikisha idadi ya wajumbe anayohitaji ili kupata uteuzi wa chama chake ya kuwania nafasi ya urais wa Marekani.
Idadi hiyo imefikiwa katika majumuisho yanayofanywa na wakala wa habari Associated Press.
Taarifa hizi zinakuja kabla ya kinyang'anyiro cha leo katika majimbo sita, ikiwemo California.
AP imesema idadi hiyo imefikiwa baada ya ushindi wa Clinton dhidi ya mshindani wake Bernie Sanders huko Puerto Rico mwishoni mwa juma na kuongezeka kwa idadi ya wajumbe ambao wanaruhusiwa kumuunga mkono mtu yeyote wanaemtaka.BBC
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT