TANZANIA:TUME YA UCHAGUZI YARUDISHA $5m | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Wednesday, 8 June 2016

TANZANIA:TUME YA UCHAGUZI YARUDISHA $5m

Image copyrightSTATEHOUSE TANZANIA
Image captionDamian Lubuva na rais John Magufuli
Tume ya uchaguzi nchini Tanzania TEC imerudisha takriban dola milioni 5 kwa serikali baada ya kutotumika katika uchaguzi wa mwaka jana.
Mwenyekiti wa tume hiyo Damian Lubuva alimkabidhi rais John Pombe Magufuli fedha hizo.
Bw Lubuva amesisitiza kuwa uchaguzi uliendeshwa kwa njia nzuri bila fedha hizo.
''Bw Rais ,tulikuwa wagumu lakini tulifanikiwa kufanya kazi zetu vzuri.Kwa hivyo hizi zilizosalia hazimaanishi kwamba kazi yetu haikuafikia mahitaji yake''.
Rais Magufuli ameitaja hatua hiyo kuwa ya kizalendo.
''Mungezificha fedha hizi na kusema kwamba zilitumika zote ,ama hata kusema hazikutosha na hakuna mtu angewauliza''.
Rais Magufuli ameamrisha fedha hizo kutumika kujenga afisi za tume hiyo.
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT