Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, amasema kuwa baada ya mazungumzo na viongozi wa kidini na maspika kutoka kamati za bunge zote mbili, kamati itabuniwa kusuluhisha mvutano uliopo kuhusu tume ya uchaguzi.
Maandamano ya hivi majuzi ya upinzani kupinga tume ya uchaguzi nchini Kenya, ambayo inalaumiwa kwa kupendelea yamegeuka na kuwa yenye ghasia.
Makabiliano na polisi siku ya Jumatatu katika mji wa magharibi wa Kisumu, yalisababisha vifo vya watu wawili.
Jana, waziri wa mambo ya ndani nchini Kenya, alipiga marufuku maandamano yote yanayohusu suala hilo.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT