Ndege ya shirika la EgyptAir ambayo ililazimika kutua nchini Uzbekistan kutokana na udanganyifu wa kuwepo kwa bomu, imeruhusiwa kuendelea na safari yake kutoka Cairo kwenda Beijing.
Abiria wote 118 na wafanyakazi 17 waliokuwa ndani ya ndege hiyo, waliondolewa katika uwanja wa kimataifa wa Urgench.
Ndege hiyo ilisakwa na maafisa wa usalama wa Uzbek lakini hakuna kilipuzi kilichopatikana.
Wiki tatu zilizopita ndege ya EgyptAir iliyokuwa ikitoka mjini Paris kwenda Cairo ikiwa na abiria 66 ilianguka katika bahari ya Mediterranean.
Chanzo cha ajali hiyo bado hakijulikani lakini maafisa nchini Misri wanadai kuwa ajali hiyo huenda ilisababishwa na shambulizi la kigaidi.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT