Waziri wa utalii nchini Brazil , Henrique Alves,amejiuzulu siku moja baada ya kushtumiwa kwamba aliitisha hongo kuchangia kampeni yake kutoka kwa shirika kubwa la serikali lililo kwenye biashara ya mafuta Petrobras.
Anakuwa waziri wa tatu kujiuzulu kutoka kwa serikali ya rais Michel Temer kutokana na kashfa hiyo.
Hata hivyo bwana Henrique Alves amekana madai hayo ya ufisadi.
Jumatano ,mahakama kuu imetoa ushaidi kutoka kwa mmoja wa wakuu wa Pretrobas, Sergio Machado ambaye amewahusisha wanasiasa ishirini mashuhuri akiwemo raisi Temer ambaye pia amepinga kuhusika kwake na harakati hizo zisizo halali.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT