Zaidi ya maafisa 50 kutoka wizara ya mambo ya nje wa Marekani wamesaini barua kutoka ofisi hiyo inayoikashifu sera ya rais Obama kuhusu Syria.
Wanasema Marekani ingefanya mashambulio ya kulenga jeshi la rais Assad ili kumkomesha kutoivunja mikataba ya kusitisha mapigano nchini humo.
Wanasema bila kufanya hivyo utawala huo wa Damascus hautahisi umuhimu wa kutilia maanani majadiliano ya amani.
Mwandishi wa BBC anasema barua hiyo imedhihirisha zaidi migawanyiko ndani ya serikali na huenda ikawashawishi watunga sera wa nchi hiyo kuhusu kutafuta njia nyenginezo za vipi ikabiliane na mzozo wa Syria na hasa kulikabili kundi la wanamgambo wa IS.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT