bongo satellite.: Habari za Kitaifa-Tanzania.
Breaking News
Loading...
Showing posts with label Habari za Kitaifa-Tanzania.. Show all posts
Showing posts with label Habari za Kitaifa-Tanzania.. Show all posts

Thursday, 22 September 2016

WABUNIFU MAJENGO NA WAKADIRIAJI MAJENZI WAASWA KUUNGANA.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na wadau wa sekta ya ubunifu majengo na ukadiriaji majenzi wakati wa Ufunguzi wa Semina ya 26 ya wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi,Jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akikabidhi cheti kwa mmoja wa wanafunzi wa shule za sekondari walioshiriki uandishi wa insha kuhusu sekta ya ubunifu majengo na ukadiriaji majenzi wakati wa Ufunguzi wa Semina ya 26 ya wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi,Jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akikabidhi cheti kwa mmoja wa wanafunzi wa shule za sekondari walioshiriki uandishi wa insha kuhusu sekta ya ubunifu majengo na ukadiriaji majenzi wakati wa Ufunguzi wa Semina ya 26 ya wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi,Jijini Dar es salaam.
 Msajili wa Bodi ya Usajili ya Wabunifu majengo na Wakadiriaji majenzi (AQRB) Arch.Jehad Abdallah akisoma taarifa ya utekelezaji wa Bodi hiyo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati wa ufunguzi wa Semina ya 26 ya Wabunifu majengo na Wakadiriaji majenzi, Jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Bodi wa bodi ya Usajili ya  Wabunifu majengo na Wakadiriaji majenzi (AQRB) Arch. Ambwene Mwakyusa akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati wa ufunguzi wa Semina ya 26 ya Wabunifu majengo na Wakadiriaji majenzi, Jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na wadau wa sekta ya ubunifu majengo na ukadiriaji majenzi wakati wa Ufunguzi wa Semina ya 26 ya Wabunifu majengo na Wakadiriaji majenzi, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa bodi Bodi ya Usajili ya Wabunifu majengo na Wakadiriaji majenzi (AQRB) mara baada ya ufunguzi wa Semina ya 26 ya wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi jijini Dar es salaam.Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchuzi na Mawasiliano.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amezungumzia umuhimu wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi kuungana ili waweze kupata fursa katika miradi mikubwa ya ujenzi itakayoanza hivi karibuni hapa nchini.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina endelevu ya 26 ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Prof. Mbarawa amesema Serikali ya Awamu ya Tano imejikita katika ujenzi wa miundombinu ya kisasa na itatoa kipaumbele kwa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi watakaoungana ili kuwa na nguvu ya kutekeleza miradi hiyo kwa viwango.
“Tunao mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa, ujenzi wa miundombinu ya kisasa mjini Dodoma, ujenzi wa makazi ya kisasa ya wananchi, vyote hivi vinahitaji wataalamu walioungana, wenye nguvu ya kufanya kazi kwa haraka na ubora unaokubalika”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Ameitaka Bodi ya Usajili ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), kujitangaza na kuwatangaza wataalamu wake ili huduma zao zitumiwe na wananchi wa ngazi zote kwa gharama nafuu.
“Shirikianeni na vyuo vinavyofundisha fani yenu ili viongeze udahili wa wanafunzi na kuhakikisha kazi zenu zinafanywa kisasa na kwa kuzingatia teknolojia”, amesema Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa ameitaka Bodi hiyo kutoa elimu ya kutosha ili kuvutia wanafunzi wengi kupenda kusoma fani hiyo na wale wanaofanya vizuri wawape motisha ya kuwasomesha katika vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi.
Akizungumza katika semina hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya AQRB, Mbunifu Majengo Ambwene Mwakyusa, amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa Bodi yake imejipanga kuhakikisha wananchi wanapata ramani za nyumba kwa bei nafuu ili kuwa na jamii yenye makazi ya kisasa.
Naye Msajili wa Bodi ya AQRB, Mbunifu Majengo Jehad Jehad amesema takribani Wabunifu majengo na Wakadiriaji majenzi 1,333 pamoja na kampuni za fani hiyo 372 zimesajiliwa na zinatoa huduma kwa mujibu wa sheria za fani hiyo.
Amebainisha kuwa Bodi yake imejipanga kuhakikisha maadili ya taaluma hiyo hapa nchini yanalindwa na atakayekiuka atafutiwa usajili na kuadhibiwa kwa mujibu wa taratibu ya bodi hiyo.
Zaidi ya miradi ya ujenzi 1,963 imekaguliwa na bodi hiyo katika maeneo mbalimbali nchini katika kipindi cha mwaka wa 2015 lengo ikiwa ni kuhakikisha ujenzi wowote unaofanyika nchini unakuwa na viwango bora.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. 
source:Mjengwa blog.

Tuesday, 20 September 2016

Salamu za Rais Magufuli kwa waathirika wa ajali mkoani Njombe.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia zilizopatwa na msiba kufuatia ajali ya basi la kampuni ya New Force iliyotokea jana Sept 19, 2016 majira  ya saa 2:00 usiku katika kijiji cha Lilombwi, kata ya Kifanya mkoani Njombe.
Ambapo watu 12 wamepoteza maisha na wengine 28 kujeruhiwa, basi hilo limepinduka katika kona ya barabara wakati likisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Songea mkoani Ruvuma.
‘Ndugu Mkuu wa mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi naomba unifikishie pole nyingi kwa wote waliopatwa na msiba, wamepoteza wapendwa wao, wamepoteza watu waliowategemea’
‘Sote tuwaombee wote waliofikwa na msiba wawe na moyo wa subira, uvumilivu na pia tuwaombee Marehemu wote wapumzishwa mahali pema peponi Amina’- Rais Magufuli.
Millard Ayo.

TUME YA MIPANGO YAENDESHA MAFUNZO KWA MAAFISA MIPANGO NA WACHUMI JIJINI MBEYA.


m1
Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri akifungua mafunzo ya Mwongozo wa Uwekezaji na Usimamizi wa Miradi ya Umma yanayoendelea katika ukumbi wa Halmashauri ya jiji la Mbeya. Kushoto kwake ni Mhandisi Happiness Mgalula Naibu Katibu Mtendaji anayesimamia Klasta ya Miundombinu na Huduma na Dkt. Joihn Mduma, Mhadhiri Mwandamizi kutoka chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kulia kwa mgeni rasmi ni Dkt. Lorah Madete, Kaimu Nibu Katibu Mtendaji, anayesimamia Klasta ya Uchumi Jumla.
m3
m4
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza mgeni rasmi (hayumo pichani)
m2
Washiriki wa mafunzo hayo kutoka mikoa ya Mbeya, Ruvuma, Songwe, Iringa na Njombe wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi. 
Mjengwa Blog.

Saturday, 10 September 2016

KUELEKEA DODOMA: Rais Magufuli atakuwa wa mwisho kuhamia Dodoma.



Rais John Magufuli

Rais John Magufuli 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Rais John Magufuli atakuwa wa mwisho kuhamia Dodoma na kupokewa na watumishi wa Serikali.
Rais Magufuli akihutubia Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Julai 23 mwaka huu, mkoani hapa alitoa tamko la Serikali kuhamia Dodoma ikiwa ni utekelezaji wa uamuzi ulitolewa mwaka 1973.
Akizungumza Jumatano wiki hii, katika kipindi cha Safari ya Dodoma kilichoandaliwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Majaliwa alisema utaratibu wa kuhama umepangwa kutekelezwa kwa awamu sita.
Alisema awamu ya kwanza itaanza mwezi huu hadi Februari mwakani, ikiongozwa naye, mawaziri wote, makatibu wakuu, naibu katibu mkuu na idara angalau moja.
“Awamu ya pili itaanza Machi hadi Agosti, 2017. Katika kipindi hicho makatibu wakuu watapendekeza na kuomba fedha bungeni kwa ajili ya kazi hiyo,” alisema. Kwa utaratibu wa Bunge, mikutano ya bajeti huanza Aprili hadi Julai ili kujadili na kuidhinisha mapato na matumizi ya Serikali ya mwaka mpya wa fedha.
Majaliwa alisema awamu ya tatu itaanza Septemba hadi Februari, 2018 na zitaendelea nyingine, ya mwisho ikiwa mwaka 2020.
Akizungumzia miundombinu, Majaliwa alisema Dodoma ina barabara za kutosha, nyingi zikiwa za lami na hata zisizo za lami zinapitika vizuri.
Majaliwa alisema kuna barabara ya kuunganisha mikoa mingine kama vile Singida, Morogoro na Iringa, hivyo kuwafanya watu kuingia na kutoka mjini hapa kwa urahisi. Kwa upande wa masoko, alisema yapo makubwa yenye vyakula vya kutosha.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu), Jenista Mhagama hivi karibuni alisema ujenzi wa makazi, uzio na ofisi binafsi za waziri mkuu umekamilika.
Mhagama alisema kilichobaki ni kazi ya uboreshaji wa mandhari ya eneo la makazi hayo yaliyoko Mlimwa, mjini hapa na barabara za kuunganisha kati ya makazi hayo na nyingine kubwa.
Alimwagiza Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma, Jordan Rugimbana kuhakikisha mandhari ya eneo hilo yanaboreshwa ikiwa ni pamoja na kupanda maua.
Rugimba pia alipewa jukumu la kusimamia ujenzi wa barabara zinazounganisha makazi hayo na nyingine zilizopo maeneo hayo.
Mwananchi.