Radio inayomilikiwa na serikali nchini India, imetangaza kuwa yamkini watu 13 wameuwawa katika maeneo ya kaskazini Mashariki mwa jimbo la Assam, baada ya watu kadhaa waliokuwa na silaha kuanza kuwamiminia risasi watu waliokuwa sokoni.
Watu 20 wamejeruhiwa, wengi wao vibaya sana.
Afisa mkuu wa polisi nchini humo, ameiambia BBC kuwa, maafisa wake wamefaulu kumuua mmoja wa mshambuliaji.
Mtu huyo aliyeuawa anasemekana kuwa mwanachama wa kundi lililo haramishwa la National Democratic Front of Bodoland.
Amesema kuwa wananchi wengi wamejeruhiwa baada ya wapiganaji hao kuwamiminia risasi na mabomu ya Gurunedi.
Walinda usalama wamezingira eneo ambalo hutokea ghasia mara kwa mara mjini Kokraj-har.
Msako dhidi ya wauwaji hao unaendelea.
Watu wa kabila la Bodo, wanataka kukatiwa jimbo lao ambalo wanalipendekeza kuitwa Bodoland.
Jimbo hilo limeshuhudia misururu ya mapigano tangu mwaka 2012.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT