Taarifa Mpya Kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Leo Ijumaa Agosti 5, 2016 | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Friday, 5 August 2016

Taarifa Mpya Kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Leo Ijumaa Agosti 5, 2016

HESLB

OFISI ZA DAR KUWA WAZI JUMAMOSI NA JUMAPILI

Ofisi za Bodi ya Mikopo zilizopo Mwenge, jijini Dar es Salaam zitakuwa wazi kwa siku mbili, Jumamosi, Agosti 6, 2016 na Jumapili, Agosti 7, 2016 kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 9:00 alasiri ili kutoa fursa muhimu kwa wadaiwa wote wa mikopo ya elimu ya juu ambao hawajaanza kurejesha mikopo kupata taarifa kuhusu madeni yao.
Bodi ya Mikopo imeshaanza kuwachukulia hatua wadaiwa wa mikopo ya elimu ya juu kwa kutangaza majina yao katika vyombo vya habari. Hatua zingine zitakazochukuliwa ni pamoja na:
i. Kufikishwa mahakamani;
ii. Kutozwa faini;
iii. Kunyimwa fursa za kupata mikopo;
iv. Kunyimwa fursa za masomo nje ya nchi; na
v. Kuzuiwa kusafiri nje ya nchi.
Nyote mnakaribishwa ili kutumia fursa hii muhimu.
‘Kuwa Mzalendo, Rejesha Mkopo wa Elimu ya Juu’
chanzo: Heslb
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT