Sehemu nyingi nchini Kenya zimekumbwa na ukosefu wa umeme asubuhi ya leo Jumamosi.
Kampuni ya usambazaji umeme nchini Kenya, imesema ukosefu huo wa umeme umesababishwa na hitilafu za kimitambo katika laini yake kuu.
Wakenya katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakisisitiza kusitisha kuondolewa kwa ukiritimba katika usambazaji wa umeme nchini humo wakisema hulo limechangia utepetevu.
Kampuni ya umeme ya Kenya Power, imesema katika taarifa yake kwamba kulikuwa na hitilafu za kimitambo zilizosababisha ukosefu wa umeme mwendo wa saa kumi na moja asubuhi katika eneo la Ol Karia.
Masaa manne baadaye, kampuni hiyo ilirekebisha hitilafu hiyo katika sehemu za magharibi na kati mwa Kenya, lakini katika mji mkuu na maeneo ya mashariki watu walikaa gizani kwa muda zaidi.
Shida kama hiyo inapotokea wafanyibiashara hutumia mbinu mbadala ya kutumia Jenereta, ingawaje bado hushuhudia hasara kwa kiwango cha juu kutokana na gharama
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT