Chama cha ANC chashindwa mji mkuu Afrika Kusini. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Saturday, 6 August 2016

Chama cha ANC chashindwa mji mkuu Afrika Kusini.

Karatasi za kupigia kura

Image captionKaratasi za kupigia kura
Katika uchaguzi wa serikali za mitaa wa Afrika Kusini, chama tawala cha ANC, kimeshindwa na Democratic Alliance, katika eneo lenye mji mkuu,Pretoria.
Matokeo ya mwisho ya eneo hilo la Tshwane, yanaonesha kuwa chama cha Democratic Alliance kimepata asilimia 43 ya kura na ANC asilimia 41.
Chama cha Democratic Alliance kitalazimika kuunda serikali ya mseto kuongeza udhibiti katika eneo.
Vyama viwili vikuu pia vinakaribiana kudhibiti Johannesburg, mji mkubwa kabisa nchini humo.

ANC imepata matokeo mabaya zaidi tangu kuingia madarakani, baada ya utawala wa ubaguzi wa rangi kumalizika.
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT