August 4, 2016
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom ambao ni wadhamini wakuu wa Ligi Kuu sokaTanzania bara msimu wa 2016/2017, wamekabidhi vifaa kwa timu zote 16 zitakazoshiriki Ligi Kuu msimu wa 2016/2017, Vodacom wamekabidhi vifaa vyenye thamani ya jumla ya Tsh milioni 514.
Vifaa hivyo vya timu za Ligi Kuu na marefa watakaochezesha mechi za Ligi Kuu vilikabidhiwa na mkuu wa masoko wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Nandi Mwiyombella, baadhi ya vifaa vilivyokabidhiwa ni jezi za nyumbani na ugenini kwa timu zote, viatu vya mazoezi na mechi, gloves, nguo za mazoezi na vilinda ugoko.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT