Rais wa serikali ya Mpito ya Brazili amesema anaamini kwamba Wabrazil watarudisha tena furaha yao, michezo ya Olimpiki ikianza rasmi leo mjini Rio De Janeiro.
Michel Temer amesema Brazil kuwa mwenyeji wa michezo hiyo ya Olympiki, licha ya misukosuko ya uchumi na kisiasa inayowakabili ni kuthibitisha uwezo wa nchi hiyo, kukabiliana na vikwazo.
Ulinzi umeimarishwa mjini Rio, kuweza kuzuia ghasia zinazoweza kuzushwa na waandamanaji wenye hasira juu ya gharama za mashindano hayo.
Shamra shamra za ufunguzi wa michezo hiyo katika uwanja wa Maracana zimepunguzwa kutokana na kupunguzwa kwa bajeti iliyokuwa imewekwa.
Lakini hata hivyo Waandaaji wake wameahidi kuwepo kwa sherehe zitakazovutia zaidi za kiutamaduni na nyingine tofauti.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT