Mwanandondi wa Morocco akamatwa kwa unyanyasaji Rio. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Friday, 5 August 2016

Mwanandondi wa Morocco akamatwa kwa unyanyasaji Rio.

Hassan Saada

Image copyrightAFP
Image captionHassan Saada alikuwa amepangiwa kupigana kesho
Polisi mjini Rio de Janeiro wanasema wamemkamata mwanamichezo raia wa Morocco kwa tuhuma za unyanyasaji wa kimapenzi.
Mwanabondia, Hassan Saada, anatuhumiwa kuwanyanyasa wafanyakazi wawili wa kike wa kufanya usafi katika Olympic Village, eneo wanamoishi wanamichezo, siku ya Jumatano.
Jaji ameagiza mwanamichezo huyo azuiliwe kwa siku 15 huku polisi wakifanya uchunguzi wao.
Saada alipangiwa kupigana pambano lake la kwanza dhidi ya Mehmet Nadir wa Uturuki hapo kesho.
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT