Nyota wa tenisi Novak Djokovic alitokwa na machozi baada ya kushindwa kwenye raundi ya kwanza katika mashindano ya mchezaji mmoja mmoja Michezo ya Olimpiki Rio.
Djokovic alishindwa na raia wa Argentina Juan Martin Del Potro.
Mserbia huyo, ambaye pia alishindwa na Del Potro mchuano wa kutafuta mshindi wa nishani ya shaba michezo ya London 2012, alishindwa tena na mwanatenisi huyo kwa 7-6 (7-4) 7-6 (7-2).
Djokovic, 29, ambaye ameorodheshwa mchezaji bora duniani, alitokwa na machozi akiondoka uwanjani baada ya mchezo huo uliodumu saa mbili na nusu.
Del Potro atakutana na Mreno Joao Sousa raundi ya pili Jumatatu.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT