Spika wa bunge la Seneti nchini Kenya Ekwe Ethuro, ameidhinisha mipango ya kuchunguza madai ya ukatili wa polisi wakati wa maandamano ya upinzani nchini humo siku za hivi karibuni.
Watu wawili waliuawa na wengine watano kujeruhiwa katika mji wa Magharibi wa Kisumu siku ya Jumatatu.
Risasi ilitolewa kutoka kwa mwili wa mtoto wa kiume ambaye alijikuta katikati ya maandamano.
Polisi waliwaua kwa kuwapiga risasi watu watatu katika maandamano kama hayo mwezi Mei. Wanadai kuwa walikuwa wakilijinda na kuzuia uporaji wa mali.
Bwana Ethuro amesema kuwa kamati ya ulinzi ya Seneti, itatoa ripoti ya uchunguzi wake baada ya siku sitini.
BBC
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT