UN:WALINDA AMANI WANYANYASAJI MASHAKANI. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Saturday, 12 March 2016

UN:WALINDA AMANI WANYANYASAJI MASHAKANI.

Image captionMlinda amani wa Umoja wa Mataifa
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mara ya kwanza limepitisha azimio la kusuluhisha suala la unyanyasaji ya kingono unaofanywa na walinda amani wa Umoja huo.
Azimio hilo ni chini ya mpango uliopendekezwa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon ambapo jeshi au polisi wataondolewa kutoka maeneo ambapo kuna ushahidi wa kuwepo vitendo kama hivyo.
Wanachama 14 wa baraza la ulinzi walipiga kura kuunga mkono azimio hilo isipokuwa Misri ambayo pendekezo lake la kutaka azimio hilo kufanyiwa marekebisho lilikataliwa.
Image copyrightAP
Image captionWalinda amani wa Umoja wa Mataifa
Azimio hilo la Umoja wa Mataifa linafuatia tuhuma zinazowakumba wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kote duniani.
BBC SWAHILI.
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT