Beki wa zamani wa Arsenal Emmanuel Eboue, amejiunga na timu ya Sunderland inayoshiriki ligi kuu ya England.
Eboue, mwenye miaka 32, alikuwa mchezaji huru baada ya kuondoka Galatasaray ya Uturuki mwanzoni mwa msimu huu.
Akiwa na Galatasaray kuanzia 2011, Eboue alifanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi hiyo mara 3 pamoja na makombe mengine matano.
Eboue aliichezea Arsenal kwa misimu minane baada ya kutua hapo mwaka 2004 kutoka klabu ya Ubelgiji ya Beveren na kisha kuhamia Galatasaray mwaka 2011.
Sunderland imempa mchezaji huyo mkataba wa muda mfupi ambao utamalizika mwishoni mwa msimu.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT