Shirika la uchunguzi wa jinai la Marekani FBI limeshindwa kufungua simu ya mmoja wa washukiwa wa mauaji ya San Bernadino, California, miezi miwili baada ya mauaji hayo kutekelezwa.
Mkurugenzi wa shirirka hilo James Comey amekuwa akitoa ushaidi katika kamati ya upelelezi ya seneti ya Marekani kuhusiana na mauaji hayo. Watu 14 waliuawa kwa kupigwa risasi.
Bwa Comey anasema kuwa mawasiliano yao yalikuwa ni ya siri na waliweza kutumia tekinolojia ya hali ya juu kuvuruga mitambo, hivyo kuathiri sheria kuweza kuchukua mkondo wake.
Sheria ya kuondoa ulinzi wa mawasiliano hayo bado inajadiliwa mjini Washngton ili kukabiliana na mashambulizi yaliyotokea California.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT