bongo satellite.: Siasa-Tanzania.
Breaking News
Loading...
Showing posts with label Siasa-Tanzania.. Show all posts
Showing posts with label Siasa-Tanzania.. Show all posts

Saturday, 10 September 2016

Lowassa, Maalim Seif siri nzito.


Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa (kulia)
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa (kulia) akizungumza na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kabla ya kuanza kwa kikao cha viongozi wa Ukawa kilichofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu na mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale-Mwiru. 
Siku moja baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba kuwasimanga viongozi wa Ukawa kuhusu namna walivyompokea Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na kumteua kuwa mgombea urais, viongozi hao jana walikutana katika kikao kilichotarajiwa kujadili suala hilo.
Kikao hicho cha Ukawa kimekuja zikiwa zimepita siku nne baada ya Lowassa na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kukutana nyumbani kwa Lowassa Jumatatu ya wiki hii.
Juzi, katika mahojiano na kituo cha redio cha Clouds FM, Profesa Lipumba alisema mkutano wa chama hicho ulioridhia Lowassa kuingia Ukawa ulifanyika Zanzibar bila yeye kuambiwa, kitendo kinachoonyesha kuwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad alikuwa akimzunguka.
Mbali na tuhuma hizo, kiongozi huyo alieleza kuwa hatakuwa tayari kuona CUF ikinunuliwa kwa bei chee na Lowassa au Chadema hata kama atakuwa nje ya chama hicho.
Jana jioni, viongozi wa vyama hivyo walikutana faragha kwenye ofisi za Lowassa zilizopo Mikocheni. Haikuweza kufahamika mara moja ajenda za kikao hicho lakini habari kutoka ndani ya vyama hivyo zilisema pamoja na mambo mengine kilitarajia kujadili shutuma zilizotolewa na Profesa Lipumba.
Suala jingine lililotarajiwa kujadiliwa na viongozi hao washirika wa Ukawa ni mkakati wa pamoja wa namna ya kuendesha shughuli za siasa katika kipindi ambacho imetolewa amri ya kuzuia maandamano na mikutano ya siasa.
Baadhi ya viongozi waliohudhuria kikao hicho ni mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale-Mwiru aliyewasili saa 10.56 jioni, Mwenyekiti wa Ukuta Profesa Mwesiga Baregu aliyewasili saa 11.06 akafuatiwa na Maalim Seif saa 11.13, na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe saa 11.18 jioni.
Mbali na kikao hicho, viongozi mbalimbali wa CUF, walijitokeza kumjibu Profesa Lipumba aliyejiuzulu uenyekiti katika kipindi cha mapambano ya kukiondoa madarakani chama tawala, CCM, lakini kauli ya pamoja ya viongozi hao ndiyo inasubiriwa kukata mzizi wa fitina.
Juzi, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alisema Profesa Lipumba ni “kigeugeu” huku Mbowe akisema “hakutegemea maneno hayo yangetoka kwa mtu kama Profesa Lipumba.”
Jana asubuhi akitumia kituo cha Clouds FM, Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano wa CUF, Mbarara Maharagande alisema siyo kweli kwamba Profesa Lipumba hakushirikishwa katika ujio wa Lowassa bali yeye ndiye aliyepeleka taarifa katika Baraza Kuu la chama kwamba Ukawa wamekubaliana kumsimamisha Lowassa.
“Alichokuwa anakifanya Maalim Seif ni haki yake kikatiba kushirikiana na viongozi wengine wa Ukawa. Mbona yeye alikwenda kumfuata Mzee Joseph Warioba kumshawishi agombee urais?” alihoji.
Maharagande alisema CUF walimtazama Lowassa kama sura ya kuleta mabadiliko kwa yale waliyokuwa wakiyataka katika Ukawa. “Profesa Lipumba alimtazama Lowassa kama mtu wa kawaida, lakini CUF walimtazama kama kiongozi mwenye ushawishi mkubwa kwa sababu ya uwezo wake wa kuunganisha wanasiasa,” alisema.
Pia, jana mchana Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu alisema Profesa Lipumba ambaye ni msomi ameanguka kifikra kutokana na kauli zake na ukweli uliopo.
Lissu, ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki alitoa kauli hiyo baada ya kuulizwa swali na waaandishi wa habari katika mkutano wake jana waliotaka kujua msimamo wake kutokana na matamshi aliyoyatoa Profesa Lipumba.
“Kwa kifupi ya Profesa Lipumba yasiwasumbue CUF na wala Chadema hayatusumbui. Wanaosumbuka ni wale wanaomtumia Profesa, kwa sababu ukweli uko wazi kutokana na mambo yaliyojitokeza baada ya ujio wa Lowassa,” alisema Lissu.
Alisema katika chaguzi zote ambazo Profesa Lipumba alikuwa akigombea urais, CUF Bara haikuwahi kupata viti vya ubunge zaidi ya viwili lakini mwaka jana kimepata viti 10 kutokana na ushirikiano wa Ukawa.
Lissu aliwahi kumwelezea Lowassa kuwa pamoja na shutuma nyingi anazorushiwa nchini bado ni tembo katika uwanja wa siasa ambaye “ukifumba macho yupo, ukisema hayupo, yupo pale.”
Lowassa kama “jongoo mpenda watu na watu hawampendi” alisababisha zogo kubwa ndani ya CCM wakati wa mchakato wa kuteua mgombea urais na jina lake lilipokatwa aliamua kutulia.
Kutokana na ushawishi mkubwa alionao katika jamii, Chadema walimfuata kumwomba ajiunge nao na akateuliwa kuwa mgombea urais na baadaye alinadiwa kwa vyama vinavyounda Ukawa vya CUF, NCCR-Mageuzi chini ya James Mbatia na NLD chini ya hayati Dk Emmanuel Makaidi.

Friday, 9 September 2016

Lowasa aitikisa CUF.



Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa .

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa . 
 Imebainika kwamba mgogoro unaoendelea kufukuta ndani ya CUF unabebwa zaidi na hoja dhidi ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba kuendelea kutumia jina hilo kama sababu za mvurugano unaokikabili kwa sasa.
Katika mahojiano na kituo cha redio cha Clouds FM, Profesa Lipumba amesema mkutano wa chama hicho uliomridhia Lowassa kuingia Ukawa ulifanyika Zanzibar bila yeye kuambiwa, kitendo kinachoonyesha kuwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad alikuwa akimzunguka.
Mbali na tuhuma hiyo, kiongozi huyo alieleza kuwa hatakuwa tayari kuona CUF ikinunuliwa kwa bei chee na Lowassa au Chadema hata kama atakuwa nje ya chama hicho.
Hata hivyo, madai hayo yamepingwa vikali na Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui aliyedai kuwa Profesa Lipumba ni “kigeugeu” huku Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akisema “hakutegemea maneno hayo yangetoka kwa mtu kama Profesa Lipumba.”
Katika mahojiano hayo, Profesa Lipumba alisema alijua uwepo wa mkutano huo baada ya Mbowe kumuuliza iwapo alikuwa anafahamu juu ya wito wake visiwani Zanzibar baada ya kuitwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar wakati huo, Maalim Seif.
“Hoja ya kwamba Lowassa anaweza kujiunga na Ukawa ilitokea katika kikao hicho wakati huo viongozi wa Chadema walikuwa na msimamo kwamba hakuna kumruhusu mtu mwingine kutoka nje kuja kugombea na tungechaguana sisi wenyewe,” alisema Profesa Lipumba na kuongeza: “Pamoja na kwamba Lowassa alianza kuwa na mazungumzo na Chadema, lakini suala la kuingia Ukawa endapo ataachwa na CCM lilianzia CUF.”
Profesa Lipumba alisema baada ya kukutana na Lowassa, waziri mkuu huyo wa zamani alimwambia kuwa tayari ameshafanya mazungumzo na viongozi wengine wa Ukawa... “Aliniuliza kama nilikuwa nikifahamu jambo hilo.”
Baada ya kumjibu kwamba hajui chochote katika mazungumzo ya awali, Profesa Lipumba alimtaka Lowassa kukutana na viongozi wote wa vyama vinavyounda Ukawa ili kujadili suala lake.
“Nilikuwa nakubali Lowassa aingie ndani ya Ukawa lakini sio kuwa mgombea wa urais. Kiongozi wa Taifa anahitaji kuwa na msimamo, hawezi kuwa anaongozwa na upepo tu kwamba ukitaka urais unaangalia chama gani kinaweza kukusimamisha kama mgombea,” alisema.
Sababu hizo za Profesa Lipumba dhidi ya Lowassa ni mwendelezo wa kutetea uamuzi wake wa kujiuzulu uenyekiti mapema Agosti mwaka jana licha ya kushiriki kumpokea kiongozi huyo katika umoja huo unaoundwa na vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD.
Lowassa, aliyegombea urais kupitia Ukawa katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka jana, alihamia Chadema mwishoni mwa Julai baada ya jina lake kukatwa na CCM katika mchakato uliofanikisha kupatikana kwa Rais John Magufuli kugombea kupitia chama hicho tawala.
Mwanasiasa huyo, ambaye amesimamishwa uanachama wa CUF alisema hana mpango wa kuhamia chama chochote wala kuanzisha kipya na endapo Lowassa atakuwa mgombea wa urais katika umoja watakaokuwa nao mwaka 2020 hatakuwa tayari kumuunga mkono.
Licha ya chama hicho kupata wabunge wengi katika uchaguzi huo, Profesa Lipumba alisema Lowassa hakuwasaidia kuongeza idadi ya wawakilishi hao kwa kuwa yalikuwa ni matokeo ya ujenzi wa chama walioufanya katika maeneo ya Kusini.
“Huwezi kupata ubunge ndani ya mwezi mmoja kama hakuna mtandao na chama hakiaminiki,” alisema Profesa Lipumba baada ya kuulizwa iwapo Lowassa alichangia kuongeza wabunge.
“Kama tungeweka wana-Ukawa wenyewe pekee na tukawa na umoja thabiti huenda tungefanya vizuri zaidi kuliko hata tulivyofanya, lakini jambo la msingi katika kipindi hiki ni kila mtu kuweza kujenga chama chake”.
Alisema Lowassa alikuwa miongoni mwa wajumbe wa Bunge la Katiba ambao hawakuunga mkono rasimu ya Jaji Joseph Warioba hivyo alikuwa kinyume kabisa na misingi iliyounda Ukawa.
 Bado ni mwenyekiti
Profesa Lipumba alidai kuwa yeye bado ni mwenyekiti wa chama hicho kwa kuwa mamlaka iliyomchagua haijatengua nafasi yake kwa kuthibitisha barua yake ya kujiuzulu.
Baada ya kujiuzulu mwaka jana, alisema watu wengi walimfuata wakiwamo wazee na vijana kumuomba arejee katika nafasi yake na walikwenda kwa Maalim Seif ambaye aliwauliza, je? Profesa atakubali.
“Nilipoona kuwa tuna matatizo mengi na wanachama kunitaka nirejee kwenye nafasi yangu ndipo nilipoandika barua ya kutengua barua ya awali ya kujiuzulu na kukijulisha chama kuwa naturudi katika ofisi yangu Juni 10 kwa ajili ya kuendelea na majukumu yangu ikiwa ni pamoja na kufanya uchambuzi wa bajeti ya Serikali na kutoa msimamo wa chama katika bajeti hiyo,” aliongeza: “Barua unaweza ukaitengua kabla ya maamuzi lakini baada ya maamuzi huwezi kutengua”.
Pamoja na wakosoaji kumwelezea kiongozi huyo kuwa anang’ang’ania madaraka, Profesa Lipumba  alipinga tuhuma hizo akieleza kuwa anaangalia mustakabali wa mtu ambaye ataweza kuifanya CUF kuwa chama cha kitaifa.
Hata hivyo katika mkutano mkuu wa CUF uliofanyika katika Ukumbi wa Ubungo Plaza mwezi uliopita, wanachama waliliridhia kujiuzulu kwa Lipumba, lakini walipokuwa wakijiandaa kupiga kura kujaza nafasi hiyo zilizuka vurugu zinazodaiwa kusababishwa na vijana wanaomuunga msomi huyo wa uchumi.
 CUF wamjibu
Akizungumza kwa simu jana, Mazrui alimtaka Profesa Lipumba asitafute mchawi kwa yanayoendelea kwa kuwa yeye ndiye wa kwanza kumtambulisha Lowassa na Ukawa CUF.
Alisema Profesa Lipumba alikuwa akiwaambia viongozi wa CUF kwamba utafiti uliokuwa umefanywa wakati huo, Lowassa alikuwa na uwezo wa kupata kura nyingi hivyo isingekuwa vibaya kama angekaribishwa ndani ya Ukawa.
“Makubaliano yalikuwa Dk (Willibrod Slaa) awe mgombea wa Ukawa lakini yeye (Profesa Lipumba) alianza kuvunja makubaliano kwa kutangaza kugombea urais akiwa Tabora. 
“Baada ya kupata fedha anakokujua alifanya sherehe Ubungo Plaza ya kuchukua fomu ya kugombea urais na baadaye ndiye aliyemleta Lowassa na kumsafisha kuwa ufisadi ni mfumo siyo mtu, sasa hapo nani kigeugeu?” alihoji.
Mwananchi.


Wednesday, 7 September 2016

WAZIRI MKUU NA MATUKIO BUNGENI LEO.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge  wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 7, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ms2
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa   akizungumza na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 7, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ms3
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Isimani na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 7, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ms4
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka kwenye jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Septemba 7, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)(P.T)

Tuesday, 6 September 2016

Ukawa sasa kurejea bungeni.


Dar/Mikoani. Baada ya siku 32 za kususia vikao vinavyoendeshwa na Naibu Spika Tulia Ackson, wabunge kutoka vyama vinavyounda Ukawa wameamua kurejea bungeni na kiongozi wao amesema mapambano ya kupinga ukandamizwaji na matumizi mabaya ya madaraka yatahamia kwenye chombo hicho.
Wabunge hao wamesema uamuzi wao unatokana na kutii wito wa viongozi wa dini na hekima za Spika Job Ndugai aliyeonyesha utayari wa kushughulikia madai yao.
Katika mkutano wa Bunge la Bajeti lililohitimishwa Juni 30, wabunge wa Ukawa, inayoundwa na vyama vya Chadema, NCCR Mageuzi, NLD na CUF walikuwa wakitoka ukumbini kila wakati Dk Tulia alipoongoza vikao, wakidai kuwa hawama imani naye kwa kuwa anawabagua na kukandamiza demokrasia ndani ya chombo hicho.
Na kutokana na Spika Ndugai kuwa nchini India ambako alikwenda kuchunguzwa afya yake, Dk Tulia ameongoza karibu vikao vyote vya nyakati za asubuhi na jioni na hivyo wabunge hao wa upinzani kuwa wanaingia ukumbini asubuhi na baada ya sala kusomwa wote kutoka nje kuanzia Mei 31 hadi Bunge lilipoahirishwa Juni 30.
Wabunge hao wameapa kuwa hawangeshiriki vikao vyote vinavyoongozwa na Dk Tulia hadi hapo madai yao yatakapopatiwa ufumbuzi, lakini baada ya kurejea kutoka India, Spika alieleza kwenye mahojiano na kituo kimoja cha televisheni kuwa yuko tayari kutafuta ufumbuzi wa suala hilo.
Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, James Mbatia ambaye pia ni mbunge wa Vunjo na mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, amesema kamati ya uongozi ya kambi ya upinzani imekutana na kukubaliana kusikiliza wito wa viongozi wa dini pamoja na hekima zilizoonyeshwa na Spika Ndugai.
“Tangu mwanzo tulitaka maridhiano, ambayo ni jambo muhimu. Hatuna ugomvi na Bunge, tulikuwa na ugomvi na kiti cha Spika hasa Naibu Spika. Tulikaa na viongozi wa dini tarehe 24 (Agosti) na tumekubali ombi lao. Tunarudi,”amesema Mbatia.
Amesema kauli ya Ndugai ni ya hekima na ya kiongozi ambaye amekomaa hiyo kwa kuwa hawana mgogoro na Bunge bali Naibu Spika, wamekaa wakaona inafaa kurejea bungeni wakati chombo hicho kitakapoanza Mkutano wa Nne ambao utadumu kwa takribani wiki mbili.
Kauli hiyo ya Mbatia iliungwa mkono na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe aliyetangaza kuwa wabunge wanaotokana na Ukawa watarejea bungeni rasmi kuanzia leo kuitikia mwito wa viongozi wa dini na wazee waliowaomba kufanya hivyo.
“Mapambano dhidi ya ukandamizani na matumizi mabaya ya madaraka kukandamiza upinzani tunayoyaendesha nje sasa yanarejea rasmi bungeni,” alisema Mbowe akiwataka wabunge wote wa kambi ya upinzani kuhudhuria bungeni.
Wapinzani wanaingia bungeni  wakiwa pungufu ya wabunge watano ambao wanaendelea kutumikia adhabu walizopewa katika mkutano uliopita.
Ukawa walianza kususia vikao hivyo Mei 31 baada ya kutolewa bungeni kwa madai ya kufanya vurugu wakati walipokuwa wakishinikiza chombo hicho kuahirisha shughuli zake na kujadili suala la wanafunzi 7,802 waliotimuliwa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kutokana na walimu wao kugoma wakidai malipo yao.
Hoja hiyo ilianzishwa na mbunge wa Chemba (CCM), Juma Nkamia Mei 30, lakini ilizimwa kutokana na kukosea kanuni na baadaye kudakwa na mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nasari aliyenukuu vizuri kanuni.
Lakini Naibu Spika alikataa suala hilo kujadiliwa na ndipo Ukawa walipoanza kupiga kelele hadi kiongozi huyo wa Bunge alipoamuru watolewe nje.
Baadaye wabunge hao walikutana na kuazimia kususia vikao vinavyoendeshwa na Dk Tulia.
Baada ya matukio hao, wapinzani walitaka kufanya mikutano kuishtaki Serikali kwa wananchi kuwa inakandamiza demokrasia, lakini Jeshi la Polisi likapiga marufuku na baadaye kufuatiwa na tamko la Rais John Magufuli, lililosababisha Chadema kutangaza operesheni iliyoitwa Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta), ambayo pia ilipigwa marufuku.
Marufuku hiyo ilikifanya chama hicho kutangaza maandamano na mikutano nchi nzima kushinikiza kuheshimiwa kwa Katiba na demokrasia, matukio ambayo yangefanyika kuanzia Septemba Mosi, lakini viongozi wa dini walikutana nao na Chadema ikaamua kuahirisha shughuli hiyo siku moja kabla
 Mwananchi.

Monday, 5 September 2016

Kauli ya JPM Z’bar ‘yatimua vumbi’.




Rais John Magufuli.
Rais John Magufuli. 
Dar es Salaam. Kauli za Rais John Magufuli kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar zimewaibua wasomi na wanasiasa, wakimtaka akubali kuwa visiwa hivyo vina mkwamo wa kisiasa na kuhitaji majadiliano.
Akihutubia wananchi kwenye Uwanja wa Gombani ya Kale kisiwani Pemba Ijumaa iliyopita, Rais Magufuli alisema uchaguzi umekwisha na hivyo wananchi wasitarajie kama kutakuwa na jambo jingine zaidi ya kusubiri uchaguzi mwingine mwaka 2020.
Juzi Rais Magufuli, ambaye amepiga marufuku mikutano ya siasa hadi mwaka 2020, alitoa hotuba nyingine kwenye Uwanja wa Demokrasia (zamani Kibandamaiti) kwa  wananchi wa Unguja iliyozungumzia uhasama wa kisiasa ulioibuka visiwani humo.
Rais Magufuli katika hotuba yake alimshauri Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk Ali Mohamed Shein kutoidhinisha malipo ya aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa iliyokuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), Maalim Seif Sharif Hamad kwa kuwa alikataa kumpa mkono wa salamu walipokutana kwenye mazishi ya Rais wa zamani wa Zanzibar, Aboud Jumbe Mwinyi.
Chanzo:Mwananchi.

Wednesday, 31 August 2016

UKUTA: Upinzani waahirisha maandamano Tanzania.

Viongozi wa upinzani wakati wa kikao na wanahabari Dar es Salaam

Image captionViongozi wa upinzani wakati wa kikao na wanahabari Dar es Salaam
Muungano wa vyama vya upinzani nchini Tanzania umeahirisha maandamano ya kitaifa ambayo yalikuwa yamepangiwa kufanyika kesho.
Viongozi wa upinzani, akiwemo Edward Lowassa wa Chadema, wametangaza hatua hiyo kwenye kikao na wanahabari Dar es Salaam.
Wamesema wameahirisha maandamano hayo kwa kipindi cha mwezi mmoja baada ya kusikia ombi la viongozi wa kidini na wadau wengine waliowaomba kukumbatia na kuyapa muda mazungumzo.
BBC.

Tuesday, 30 August 2016

UVCCM WAAHIRISHA MAANDAMANO YAO,WATII AGIZO LA JESHI LA POLISI.

  • Written by   
  • Agosti 22, 2016 Umoja wa Vijana wa CCM tuliutangazia umma na dunia kwamba ifikapo Agosti 31 mwaka huu tutaitisha maandamano ya amani nchi nzima yenye lengo la kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk John Pombe Magufuli kwa utendaji wenye tija, ufanisi na uliorudisha imani na matumaini kwa wananchi.
    Msimamo na dhamira ya kufanya maandamano hayo ya amani yenye maudhui na kusudio hilo, bado uko pale pale ingawaje si kwa tarehe tuliopanga na kutangaza awali yaani Agosti 31 mwaka huu.
    Jumuiya yetu kama mjuavyo ni ya Vijana wa CCM, (UVCCM) inapata malezi kwa karibu mno na Jumuiya ya Wazazi ya CCM. Wiki ya jana Mwenyekiti wa Wazazi Taifa Nd. Abdallah Bulembo alikutana na waandishi wa habari akitutaka UVCCM tuahirishe maandamano ya Agosti 31 mwaka huu hadi wakati mwingine.
    Kwa mujibu wa Katiba ya Chama Cha Mapinduzi, Jumuiya ya Wazazi ndiyo Msimamizi wa Malezi, Maadili na Adabu kwa Vijana wote nchini, sisi UVCCM tunaamini kuwa sikio halishindani na kichwa, mtoto ni mtoto kwa Wazazi wake hakui, hana jeuri wala ubishi.
    Mtoto au watoto wanaokaidi amri, ushauri au maelekezo ya Wazazi wao huitwa watukutu, wenye viburi, manunda na wasioambilika. UVCCM si watukutu, hatukufunzwa tuwe wabishi, wakaidi na wenye viburi. Tumezingatia kutii maelekezo, makatazo na maonyo , tumeambiwa tuahirishe maandamano yetu nasi tumekubali na kuheshimu mambo tuliyoaswa.
    Sambamba na hilo tumepata majibu ya barua yetu tuliyomwandikia Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP Ernes Mangu) inayotutaka tuache kufanya maandamano yetu kwa sababu Polisi wamezuia mikutano ya hadhara ya Vyama vya Siasa na maandamano nchi nzima.
    Jambo jingine ambalo limetufanya pia tuahirishe maandamano yetu ya Amani ni taarifa ya kintelejinsia iliowasilishwa na Kamati yetu ya Usalama na Maadili ya UVCCM mbele ya kikao cha Sekreteriet yetu, nayo ilipendekeza suala hilo liahirishwe kwa wakati huu hadi muda mwingine.
    Pia jambo jingine ambalo limefanya maandamano hayo tuyabatilishe ni kulipisha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ ) ambalo litakuwa katika shughuli za maadhimisho miaka 52 tokea kuanzishwa kwake.
    Wanajeshi wetu watakuwa katika kazi mbalimbali za kijeshi kwenye kambi zao na mitaani kufanya usafi wa mazingira, hivyo isingependeza na wala si heshima wakati sisi tukiandamana, wao wakifanya kazi muhimu kila mmoja wetu zinazomgusa badala yake ni vyema kuwaunga mkono jambo wanalolifanya la usafi wa mazingira.
    UVCCM tumekubali, hatutaki kuingia katika uvunjaji wa sheria hasa baaada ya kutakiwa kuahirisha na mamlaka za Kisheria hadi wakati mwingine muafaka na si wakati huu.
    Tunaelewa kwamba uamuzi wetu wa awali wa kutaka kuandamana kwa amani hata kama tungenyimwa kibali ungetugharimu, ungetusababishia madhara na pengine hasara, kwa wakati huu na kuona jambo lenyewe ni la kuipa Ari serikali katika kuhimiza Uwajibikaji, Utendaji na Usimamizi bora wa Uendeshaji wa masuala ya kiutawala.
    Tulishusha maagizo kwa Makatibu wetu wote wa Mikoa yote 32 na Wilaya 171 ya Kichama tukiwataka waandike barua katika Ofisi za Ma RPC na OCD, washirikiane ili kuratibu maandamano na kuyafanikisha kama tulivyokusudia.
    Watendaji wetu wa ngazi husika wamefuata maelekezo, wametii taratibu zetu za kiutendaji na leo tumewajulisha tena wasitishe maandamano hadi tutakapowapa tena maelekezo mengine. Tunawahimiza na kuwataka ni vyema kutii mamlaka za Kikanuni na Kisheria.
    UVCCM kwa wakati huu tumeamua kuachana na maandamano badala yake tunajikita katika matayarisho ya kuwapeleka Vijana wetu wakashiriki katika Mafunzo ya Siasa, Utawala, Uongozi, Ufundi na Ujasiriamali yatakayoanza kufanyika katika Chuo chetu kilichopo huko Ihemi Mkoani Iringa ambapo kitakuwa kielelezo na alama nzuri ya kumuunga mkono Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kwa vitendo.
    Tumewataka Makatibu wetu wa Mikoa na Wilaya kuendelea na zoezi la Uratibu na Uhakiki kwa Vijana ambao watateuliwa kushiriki Mafunzo hayo huko Ihemi.
    UVCCM tunarejea kusema tena kwamba dhamira ya maandamano yetu ya kusifu Utendaji wa Serikali ya awamu ya tano iko pale pale ila tutapanga tarehe nyingine katika wakati ujao badala ya kufanyika Agosti 31 mwaka huu kama tulivyotangaza hapo awali.
    UVCCM tunawataka Vijana wote kuendelea kuheshimu Tunu ya Amani Umoja na Mshikamo wetu kwa Taifa.
    KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
    Shaka Hamdu Shaka (MNEC)
    KAIMU KATIBU MKUU.(P.T)

    Wapinzani wamkumbuka Kikwete.


    Dar es Salaam.  Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amesema wanamkumbuka Rais mstaafu Jakaya Kikwete kwa namna utawala wake ulivyowaruhusu kufanya siasa bila kubughudhiwa.
    Akizungumza ofisini kwake jijini Dar es Salaam, amesema “Ninamkumbuka Kikwete. Ninaposema kwamba ninamkumbuka sikumbuki udhaifu wa Serikali yake, siikumbuki Serikali yake ..... Na tumemsema sana. Tulisema huyu rais ni dhaifu na mimi nilimwandika kwenye orodha ya mafisadi.”
    Katika utawala wake wa miaka 10, Rais mstaafu Kikwete alikebehiwa ndani na nje ya Bunge kwa kuitwa rais dhaifu, lakini miezi 10 tu tangu astaafu, wapinzani wake wa kisiasa wameanza kumkumbuka.
    Kikwete, ambaye alistaafu urais baada ya Rais John Magufuli kuapishwa Novemba 5, 2015, anakumbukwa na wapinzani kwa namna utawala wake ulivyoongeza kasi ya kukua demokrasia na kuukuza upinzani.

    Viongozi Chaumma waungana na JPM kuhamia Dodoma.

    

Rais John Magufuli

    Rais John Magufuli 
    Dodoma. Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) kimempongeza Rais John Magufuli kwa hatua yake ya kutekeleza azimio la kuhamishia makao makuu ya Serikali mkoani Dodoma, huku kikisema huo ndiyo ulikuwa mkakati wa chama hicho wa muda mrefu.
    Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Kayumbo Katubali alisema ujio wa Serikali bado ni wa kusuasua kuliko kama Chaumma kingeingia madarakani kwani kilikuwa na mkakati thabiti wa kuanzia Serikali yao Dodoma tangu siku ya kiapo.
    “Nampongeza Magufuli, ametuonyesha kwa vitendo siyo maneno yaliyokuwa yakisemwa na wanachama wa chama chake kwa zaidi ya miaka 40. Sisi kwenye ilani yetu ya Uchaguzi Mkuu tulipanga kuanzia Dodoma na si vinginevyo,” alisema Kabutali.
    Kabutali alisema kwenye ilani yao ya uchaguzi, ibara ya 18 walieleza Serikali yao itakuwa Dodoma baada ya kutangazwa washindi. Mwanasiasa huyo alimtaka Rais Magufuli kukamilisha mchakato wa kuhamia mjini hapa kwa kuutungia sheria ili wanasiasa wasitoe matamko yasiyo na tija.
    Kuhusu wakazi wa Dodoma alisema kuwa huenda ikawa faraja kwao kwani kwa sasa Serikali itakuwa karibu nao hivyo watapumzika manyanyaso waliyokuwa wakiyaopata wanapotafuta ardhi.
    Alisema wakazi wa Dodoma walishachoshwa na urasimu wa Mamlaka ya Uendelezaji Makao Makuu (CDA) na ndiyo maana migogoro ya ardhi ikawa haimaliziki. Aliwataka wana-Dodoma wawe makini na wasikubali kudanganywa na wajanja katika masuala ya ardhi.
    Mwananchi.

    Lipumba Aendelea Kung’ang’ania Uenyekiti Wake CUF.


    Katika hali isiyokuwa ya kawaida Prof Lipumba ameendelea Kung’ang’ania kiti cha uenyekiti wa chama chake cha CUF na kusema kikao kilichokaa jana visiwani Zanzibar na kufanya maamuzi ya kuwasimamisha uanachama, hakikuwa halali na kilikuwa nje ya katiba ya CUF, sababu mojawapo ikiwa ni kuwekwa kando kwa Naibu Katibu Mkuu Bara, Magdalena Sakaya.
    “Kikao hicho  hakikuwa halali, haiwezekani Baraza Kuu linakaa halafu Naibu Katibu Mkuu Bara hajui, wala hakujulishwa, na bado kuna wajumbe wengine hawakuhusishwa” Alisema Prof Lipumba
    Lipumba aliongeza kuwa ni kweli alijiuzulu uenyekiti, lakini baadaye aliamua kuandika barua kwa Katibu Mkuu ya kutengua uamuzi wake wa kujiuzulu na sasa yeye ndiye Mwenyekiti halali wa chama hicho.
    “Nilimuandikia barua ya kurudi kwenye nafasi yangu, akasema anasubiri ushauri wa kisheria, lakini hadi sasa hakuna kitu, hiyo inamaanisha kuwa sasa mimi naendelea na nafasi yangu, na niko ngangari kama mwenyekiti” Alisema Prof Lipumba.
    Aidha aliongeza kuwa alitaka kujieleza katika mkutano mkuu mbele ya wanachama, lakini mkutano ule ukavurugwa.
    Kuhusu kuwepo kwa tofauti kati yake na Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad, Prof Lipumba amesema kuwa huenda kuna tofauti kwa kuwa mara nyingi huwa hamuelewi jinsi anavyokiendesha chama bila kufuata misingi ya kidemokrasia.
    “Katibu Mkuu anamdharau na hampi heshima yake Naibu Katibu Mkuu Bara, mara nyingi huamua mambo yake bila kushirikisha viongozi wengine, halafu sasa anataka kufukuza wanachama, huwezi kuwa na chama halafu ufukuze wanachama, wanachama wanatafutwa duniani kote, halafu wewe unawafukuza, hizo ni dalili za uongozi wa kiimla, kuongoza chama unapaswa kujali demokrasia na siyo kuwa dikteta ndani ya chama” Amesema
    Kuhusu Julius Mtatiro kuwa mwenyekiti mpya wa Kamati ya Uongozi, Lipumba amesema kuwa hatambui maamuzi hayo, na wala hamtambui Mtatiro kama kiongozi wa chama hicho bali mjumbe wa Mkutano Mkuu, nafasi ambayo yeye ndiye aliyempa.
    “Mtatiro hawezi kuwa mwenyekiti, mimi ndiye mwenyekiti wa chama, Mtatiro alishindwa hata kuongoza mkutano mkuu, ukavurugika, hawezi, simtambui”
    by Kurasa Mpya.

    Monday, 15 August 2016

    CUF yampiga chini rasmi Profesa Lipumba.


    Lipumba-Prof
    ALIYEKUA Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ametoswa rasmi kuwania nafasi hiyo katika uchaguzi wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika Agosti 21 mwaka huu, kupitia Mkutano Mkuu Maalumu.
    Hali hiyo imebainika baada ya kuteuliwa kwa majina ya watu tisa kwa ajili ya kuwania nafasi hiyo ya uenyekiti, huku jina la Profesa Lipumba likikosekana katika orodha hiyo.
    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa chama hicho, Shaweji Mketo, pia majina manne yameteuliwa kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti likiwamo jina la Dk. Juma Duni Hajji ambaye anatetea nafasi yake.
    Mwishoni mwa mwaka jana, Dk. Hajji  alijiuzulu nafasi hiyo na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambapo aliteuliwa kuwa mgombea mwenza wa urais akiwa na Edward Lowassa aliyeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi ( Ukawa).
    Katika taarifa hiyo, Mketo alisema nafasi nyingine zinazowaniwa kwenye uchaguzi huo ni pamoja na nafasi nne za wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa  wa Kanda ya Nyanda za juu Kusini ambapo mjumbe yeyote anaweza kugombea kutoka kanda hiyo na nafasi moja ya mjumbe kutoka Kanda ya Kati ambapo mjumbe yeyote wa Mkutano Mkuu Taifa kutoka kanda hiyo anaweza kugombea.
    Alisema nafasi moja ya mjumbe kutoka Kanda ya Ziwa ambayo ni ya mwanamke anaweza kugombea mjumbe yoyote na nafasi moja kutoka Kanda ya Kaskazini ambapo  mjumbe yeyote kutoka kanda hiyo pia anaweza kugombea.
    Aliyataja majina tisa ya wanaowania nafasi ya mwenyekiti na taaluma zao kwenye mabano kuwa ni pamoja na Abdul Omary Zowo (Mhandisi wa Ndege za Kivita), James Mahangi (Maabara), Joseph Rhobi (Fundi Seremala), Juma Nkumbi (Mtaalamu wa Kompyuta), Salum Barwany (Fundi Magari), Selemani Khatibu, Twaha Taslima (Mwanasheria), Zuberi Kuchauka (FTC Mechanical) na Riziki Mngwali (Usuluhishi wa migogoro).
    Mketo alisema, majina manne ambayo yanawania nafasi ya makamu mwenyekiti na taaluma zao kwenye mabano ni pamoja na Dk. Juma Ameir Muchi (Daktari), Juma Duni Hajji (Mchumi), Mussa Hajji Kombo na Salim Abdallah Bimani.
    Alisema, Mkutano Mkuu Maalumu wa kupitisha majina hayo unatarajiwa kufanyika Agosti 21 mwaka huu, jijini Dar es Salaam ambao utaweza kuziba nafasi zilizoachwa wazi
    Alisema kuwa chama hicho kilitoa utaratibu wa uchukuaji wa fomu hizo za kuomba nafasi za uongozi ambapo wagombea walitakiwa kwenda kwenye ofisi za  makatibu wa wilaya kwa ajili ya kuchukua fomu hizo, hali iliyosaidia kufanikisha zoezi hilo.
    Alisema kutokana na hali hiyo, siku ya mwisho ya kuwasilisha taarifa za wagombea hao kwenye ofisi za makatibu wa wilaya ilikua Agosti  10 mwaka huu.
    “Naomba niwashukuru wanachama na viongozi wetu katika ngazi zote nchini kwa kuhamasisha wanachama wenzao ambao wameweza kuchukua fomu za kuwania nafasi ya uongozi ndani ya chama.

    Ukawa wakumbuka mitikisiko.

    Chadema+pic
    Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema uchaguzi wa mwaka jana haukuwa rahisi kwani Ukawa ilipitia katika mitikisiko mitatu.
    Mtikisiko wa kwanza ni mchakato wa kumpata mgombea urais wa Ukawa ambao haukuwa rahisi kutokana na hali halisi ya uchaguzi huo, mtikisiko wa kuondoka kwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na mwisho ni  kutangazwa kwa matokeo ya urais.
    Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi mwishoni mwa wiki, Mrema amesema mchakato wa kumpata mgombea urais ndani ya Ukawa ulikuwa mgumu kutokana na mazingira yalivyokuwa kwa sababu vyama vya Chadema na CUF, kila kimoja kilikuwa na uwezo kutoa mgombea wa urais.
    “Ninakumbuka mara kadhaa tuliwaita waandishi wa habari ili tumtangaze, lakini tuliahirisha kutokana na ugumu uliokuwapo katika mchakato huo,” amesema.
    Mrema ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ndogo ya kuandaa mapokezi ya kumkaribisha, Edward Lowassa aliyetoka CCM.
    Lowassa alijiengua CCM na kujiunga na Chadema siku chache baada ya jina lake kukatwa katika mchakato wa kuwania urais mkoani Dodoma.
    Mapema kabla ya jina lake kukatwa, Lowassa alikaririwa akisema hakuna wa kumkata jina lake, na kama akikatwa, kwanini akatwe wakati katika mapambano hakuwahi kushindwa.
    Mrema amesema, kabla ya mchakato huo wa kumpata mgombea urais haujatulia, Ukawa ikapata mtikisiko wa kuchomoka kwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Lipumba na baadaye Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Slaa.

    Saturday, 13 August 2016

    Mrema: CCM na TLP iwe UKAWA mpya.

    mremaa
    Mwenyekiti wa TLP, Augustino Mrema amesema pamoja na Rais John Magufuli kufanya kazi vizuri, hawezi kurejea CCM na badala yake amependekeza vyama hivyo viwili viunde ushirikiano wao kama ilivyo kwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
    Waziri huyo wa zamani wa mambo ya ndani, pia amesema kuna haja ya suala la maandamano na mikutano ya kisiasa kuundiwa kanuni ili kuondoa malalamiko ya vyama vya upinzani kuzuiwa kutekeleza haki hiyo ya kikatiba.
    Mrema, ambaye hivi karibuni aliteuliwa na Rais Magufuli kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Msamaha kwa Wafungwa (Parole), alitoa kauli hiyo jana wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa na kituo cha redio cha Clouds FM.
    Alikuwa ameulizwa na mmoja wa wasikilizaji wa kipindi hicho kwa nini asirejee CCM kama anaridhika kuwa Rais Magufuli anatekeleza yale ambayo alitaka yafanyike lakini hayakufanyika hadi akaamua kuisaliti Serikali ya Awamu ya Pili na kuihama CCM na kwenda NCCR-Mageuzi kabla ya kuanzisha chama cha TLP.
    Mrema alijibu swali hilo kwa kuanza kueleza historia yake na mambo aliyofanya wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani katika kupambana na uhalifu na kwamba alipoona anatofautiana na Serikali aliamua kujitoa.
    Alisema CCM chini ya Serikali inayoongozwa na Rais Magufuli inafanya vizuri kwa kutekeleza yale aliyokuwa akiyataka wakati akiwa waziri.
    Alisema Rais Magufuli anatoa ushirikiano kwa kila mtu, hivyo atakuwa bega kwa bega kumsaidia kiongozi huyo aliyedai anatekeleza majukumu yake uwazi.
    “Hiyo Ukawa nyingine siipendi kwa sababu haijui inataka kufanya nini.”
    Mrema, ambaye alikuwa Mbunge wa Jimbo la Vunjo kwa tiketi ya TLP mwaka 2010 hadi 2015, alisema ataendelea kumwamini Rais Magufuli kutokana utendaji kazi wake kazi mzuri, ikiwamo kupambana na ufisadi, kazi ambayo alisema anapenda aone ikifanyika.
    Akizungumzia uamuzi wa Rais Magufuli kupiga marufuku maandamano na mikutano ya kisiasa. Mrema alisema agizo hilo ni sahihi kwa sababu hakuna haja ya mikutano wakati uchaguzi ulishapita. Lakini alipoulizwa kama Serikali ingezuia mikutano na maandamano wakati alipoihama CCM mwaka 1995, Mrema, ambaye alivuta hisia za wengi wakati huo alisema katika kipindi hicho Rais hakuwa Magufuli.
    Alisema kama Magufuli angekuwa ni Rais wakati huo na anatekeleza hayo aliyokuwa anataka, angekubaliana na uamuzi wa kuzuia maandamano.
    Mwananchi

    Chadema wagawana bendera za Ukuta.

    ukuta
    Chadema imeanza maandalizi ya operesheni ya kupinga uvunjaji wa katiba na sheria nchini iliyopangwa kufanyika Septemba Mosi kwa kugawa bendera za chama hicho kwa viongozi mbalimbali wa Kanda ya Pwani.
    Kanda ya Pwani ya chama hicho inajumuisha mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. Bendera hizo ni kwa ajili ya kuweka kwenye ofisi, kwenye nyumba na maeneo ya biashara na kupeperusha kwenye magari.
    Katibu wa Kanda ya Pwani, Casimir Mabina amewaambia waandishi wa habari kwamba wanafanya hivyo kama ishara ya kuunga mkono tamko la Kamati Kuu ya Chadema ya kufanya maandamano ya amani na mikutano nchi nzima.
    “Chadema Kanda ya Pwani tunaunga mkono kauli na tamko la Kamati Kuu ya Chadema la kupinga kwa nguvu zote, msimamo wa utawala huu wa awamu ya tano wa kukandamiza demokrasia. Sisi Kanda ya Pwani tutashiriki kikamilifu katika operesheni hiyo,” amesema Mabina.
    Amewataka wafuasi wa chama hicho kanda hiyo kutundika kila eneo bendera watakazopewa katika kile alichokiita amshaamsha kuelekea Septemba Mosi.
    “Mwenye gari aweke bendera, mwenye ofisi, mwenye duka, kila kona tandazeni bendera za chama kama ishara ya kuunga mkono uamuzi wa chama chetu wa kupinga uminywaji wa demokrasia unaofanywa na serikali ya awamu ya tano,” alisema.
    Hata hivyo, Rais John Magufuli ameonya mara kadhaa kwamba asijaribiwe, mikutano ya siasa hadi mwaka 2020. Mikutano pekee aliyoruhusu ni ya ndani na wabunge katika majimbo yao lakini si ya wanasiasa.
    Chadema inasema tamko hilo la Rais Magufuli ni kinyume cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano, Sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992, na Kanuni za maadili ya vyama vya siasa za mwaka 2007, kwani zinaruhusu mikutano na maandamano kwa ajili ya kutafuta wanachama na kunadi sera mradi watoe taarifa polisi kwa ajili ya ulinzi. Katika siku za hivi karibuni, mikutano kadhaa ya Chadema imesambaratishwa na Jeshi la Polisi.
    Katika mkutano huo na waandishi wa habari, Mabina amesema anashangaa wakati Rais Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM anakataza wapinzani kuandamana, wafuasi na wanachama wake wameonekana wakifanya maandamano kutoka uwanja wa ndege kuelekea yalipo makao makuu ya chama chao.
    “Nasema haya kutokana na taarifa iliyotolewa na Ole Sendeka kuwa Rais alikuwa akifanya ziara ya chama ambayo ilianzia Dodoma makao makuu ya CCM baada ya kuchaguliwa kushika wadhifa wa mwenyekiti wa Taifa… leo (jana) amemalizia mtaa wa Lumumba zilipo ofisi ndogo za chama,” alisema
    Kwa mazingira hayo, Mabina alisema Chadema Kanda ya Pwani inaunga mkono operesheni hiyo iliyopewa jina la Ukuta na kuwa watahakikisha inafanyika kama ilivyokusudiwa na kwamba kwa umoja wao watasimama imara.
    “Kutokana na Serikali ya awamu ya tano kuonekana kukandamiza demokrasia nchini, sisi Chadema Kanda ya Pwani tumeazimia kushiriki kwa nguvu zote kwenye operesheni Ukuta” alisema.
    Aliongeza kuwa nia yao ni kuungana na wenzao nchi nzima kupinga ukandamizaji wa demokrasia na uhuru wa vyama vya upinzani kufanya siasa kama Katiba na sheria za nchi zinavyoruhusu.
    Mwananchi

    Friday, 12 August 2016

    Mambo 10 aliyozungumza Rais Magufuli baada ya kutua Dar leo.

    August 12 2016 Rais wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli alipokelewa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere Dar es salaam akitoke mkoani Mwanza katika ziara yake akiwa kama mwenyekiti wa Chama Cha Mapunduzi (CCM) kisha baadae kwenda kuhutubia katika ofisi ndogo za chama Lumumba.