Kauli ya JPM Z’bar ‘yatimua vumbi’. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Monday, 5 September 2016

Kauli ya JPM Z’bar ‘yatimua vumbi’.




Rais John Magufuli.
Rais John Magufuli. 
Dar es Salaam. Kauli za Rais John Magufuli kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar zimewaibua wasomi na wanasiasa, wakimtaka akubali kuwa visiwa hivyo vina mkwamo wa kisiasa na kuhitaji majadiliano.
Akihutubia wananchi kwenye Uwanja wa Gombani ya Kale kisiwani Pemba Ijumaa iliyopita, Rais Magufuli alisema uchaguzi umekwisha na hivyo wananchi wasitarajie kama kutakuwa na jambo jingine zaidi ya kusubiri uchaguzi mwingine mwaka 2020.
Juzi Rais Magufuli, ambaye amepiga marufuku mikutano ya siasa hadi mwaka 2020, alitoa hotuba nyingine kwenye Uwanja wa Demokrasia (zamani Kibandamaiti) kwa  wananchi wa Unguja iliyozungumzia uhasama wa kisiasa ulioibuka visiwani humo.
Rais Magufuli katika hotuba yake alimshauri Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk Ali Mohamed Shein kutoidhinisha malipo ya aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa iliyokuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), Maalim Seif Sharif Hamad kwa kuwa alikataa kumpa mkono wa salamu walipokutana kwenye mazishi ya Rais wa zamani wa Zanzibar, Aboud Jumbe Mwinyi.
Chanzo:Mwananchi.

Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT