Orodha mauaji dada’ke Bilionia Msuya yaongezeka | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Monday, 5 September 2016

Orodha mauaji dada’ke Bilionia Msuya yaongezeka

Dar es Salaam. Idadi ya washtakiwa katika kesi ya mauaji ya Aneth Msuya ambaye alikuwa dada wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, Erasto Msuya maarufu bilionea Msuya, imeongezeka na kufikia wawili baada ya mwingine kuunganishwa nayo.
Awali, Agosti 23, mwaka huu mshtakiwa Miriam Mrita (41) ambaye ni mke wa bilionea huyo alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shtaka la mauaji ya Aneth aliyekuwa wifi yake.
Hata hivyo, juma moja baadaye, mfanyabiashara wa jijini Arusha, Revocatus Evarist (40),  alipandishwa kizimbani katika Mahakama hiyo na kuuunganishwa na Miriam kwenye kesi hiyo.
Evarist alipandishwa kizimbani mahakamani hapo Ijumaa iliyopita na kusomewa shtaka la mauaji ya Aneth na Wakili wa Serikali, Diana Lukondo.
Mwananchi.

Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT