Wabunge ‘kumweka kati’ Dk Tulia. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Monday, 5 September 2016

Wabunge ‘kumweka kati’ Dk Tulia.



Naibu Spika, Dk Tulia Ackson


Dar es Salaam. Kambi rasmi ya upinzani imepanga kufanya vikao vya kujadili suluhu ya kudumu ya mgogoro na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson uliosababisha wabunge wanaounda Ukawa kususia vikao vinavyoendeshwa na kiongozi huyo.
Vikao hivyo vinapangwa kufanyika wakati mkutano wa nne ukianza rasmi kesho, baada ya kuahirishwa mwishoni mwa Juni mwaka huu wakati wa mkutano wa Bajeti.
Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia alieleza jana kuwa uamuzi wa kufanya vikao hivyo umefikiwa baada ya upinzani kukaa na viongozi wa dini Agosti 24   ili kutafuta suluhu ya kudumu.
“Kikao cha kwanza tutakaa kamati ya uongozi ya wabunge wa upinzani kujadili suala hilo, baadaye tutamaliza na kikao cha wabunge wote ili kubaini njia endelevu za kumaliza jambo hilo,” alisema Mbatia ambaye ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi.
Mwananchi.
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT