Kimbunga Hermine chakumba pwani ya Florida. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Friday, 2 September 2016

Kimbunga Hermine chakumba pwani ya Florida.

Picha ya NOAA iliyopigwa Septemba 1, 2016

Image copyrightNOAA
Image captionHermine ndicho kimbunga cha kwanza kukumba Florida katika karibu siku 4,000
Kimbunga Hermine kimefika maeneo ya kaskazini mwa Florida, Marekani na kuwa kimbunga cha kwanza kukumba jimbo hilo tangu mwaka 2005.
Kimbunga hicho kilifika katika ghuba ya Florida mapema Ijumaa kikiwa katika kitengo nambari moja, na kusababisha mvua kubwa na upepo.
Gavana Rick Scott ametangaza hali ya tahadhari katika kaunti 51 za jimbo hilo huku wakazi wakijiandaa kwa athari za kimbunga hicho.
Upepo ulioandamana na kimbunga hicho ulifikia kasi ya 80mph (130km/h) Alhamisi, kwa mujibu wa taasisi ya taifa ya Marekani inayofuatilia vimbunga.
Maafisa katika mji mkuu wa jimbo hilo Tallahassee, ambao utakumbwa na kimbunga hicho, wamesema karibu nyumba 70,000 kwa sasa hazina umeme.
Kimbunga cha mwisho kukumba Florida kilikuwa Wilma Oktoba 2005, na kilitokea mwaka ambao kimbunga cha Katrina kilitokea.
Kimbunga hicho kilisababisha vifo vya watu watano na uharibifu wa karibu $23bn (£17bn).
Miti iliangushwa na upepo mkali CarabelleImage copyrightAP
Image captionMiti iliangushwa na upepo mkali Carabelle
Mji wa Tarpon Springs unajiandaa kukumbwa na mafurikoImage copyrightAP
Image captionMji wa Tarpon Springs unajiandaa kukumbwa na mafuriko
"Hili linatishia maisha. Hatujashuhudia kimbunga katika miaka mingi," Gavana Scott amesema.
Ameongeza kwamba maafisa 8,000 wa usalama na uokoaji wamewekwa tayari kusaidia raia.
bbc.
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT