Timu ya taifa ya kina dada ya Zimbabwe imecharazwa 6-1 na timu ya taifa ya Ujerumani kwenye mechi zilizochezwa siku ya kwanza ya michezo ya Olimpiki mjini Rio de Janeiro, Brazil.
Ujerumani, waliokuwa mabingwa 2000, 2004 na 2008, walikuwa na kibarua rahisi dhidi ya timu hiyo ya Afrika. Wakati mmoja, mabao yalikuwa 2-1 lakini mabinti hao wa Zimbabwe walionekana kulemewa na uchovu dakika za mwisho mwisho na wakabebeshwa magoli matatu katika kipindi cha dakika 16.
Michezo ilianza kwa mechi kati ya Sweden na Afrika Kusini ambapo Sweden walishinda 1-0.
Baadaye, wenyeji Brazil walilaza Uchina 3-0. Uwanja wa Olimpiki, wenye uwezo wa kupokea mashabiki 60,000, ulikuwa hauna mashabiki wengi mechi ya kwanza, lakini zaidi walifika kabla ya mechi hiyo ya Brazil.
Janine Beckie wa Canada naye alifunga bao sekunde 20 pekee baada ya mechi yao dhidi ya Australia kuanza, na kuweka rekodi ya bao la kasi zaidi lililofungwa katika historia ya soka ya wanawake Olimpiki.
Marekani wanapigiwa upatu ksuhinda michuano hiyo.
BBC SWAHILI.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT