Na: Frank Shija, MAELEZO
Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam inakusudia kuruhusu baadhi ya maduka makubwa kutoa huduma zaidi ya muda wa kawaida wa maduka kufungwa ili kutoa fursa kwa wafanyakazi kupata huduma hiyo pindi wanapotoka makazini.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda alipomwakilisha Makamu wa Rais kwenye hafla ya Futali iliyoandaliwa na Benki ya NMB jana jijini Dar es Salaam.
Makonda alisema kuwa kusudio hilo linatokana na changamoto ya upatikanaji wa nafasi ya kupata huduma hiyo kwa wafanyakazi kwani uchelewa kutoka maofisini jambo lilalosababisha baadhi ya wafanyabiashara kupeleka bidhaa zao huko huko ofisini.
Aliongeza kuwa amekusudia kufanya mambo muhimu matatu katika kipindi hiki cha mwenzi mtukufu wa ramadhani ambapo aliyataja mambo hayo kuwa ni kuongeza muda wa kufunga maduka hasa yale makubwa (malls), kupiga marufuku uvutaji wa sigara katika maeneo ya umma na kupambana na watumiaji wa usafiri wa pikipiki wanaokiuka sheria ya matumizi ya Kofia ngumu (helmet).
“Nimekusudia kufanya mambo muhimu matatu ndani ya mwezi huu mtukufu wa ramadhan, niwadokeze tu kuwa mambo hayo ni pamoja na kuongeza muda wa kufanya biashara kwa maduka makubwa (shopping malls), kupiga marufuku uvutaji wa sigara katika maeneo ya umma na kupambana na wavunjifu wa sheria ya matumizi ya helmet.” Alisema Makonda.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Tanzania Bibi. Ineke Bussemaker alisema kuwa wao kama Taasisi ya Kifedha imekuwa na desturi ya kuwajali wateja wao hivyo wanatumia fursa hii kushiriki pamoja na wateja wao walio katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan ili kuwatia moyo wakustahilifunga hiyo muhimu katika uislamu.
Aidha aliongeza kuwa NMB itaendelea kushirikiana na jamii mbalimbali katika kuhakikisha inasaidia pale panapohitajika msaada wao kama ambavyo wamekuwa wakitoa misaada katika kuchangia huduma za kijamii kama vile madawati.
mjengwa blog.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT