Moja ya habari iliyoripotiwa ni hii kutoka gazeti la habari leo, yenye kichwa cha habari‘Wenye kisukari watamani uhaba wa sukari uendelee’
#HabariLEO Wenye kisukari watamani uhaba wa sukari uendelee kutokana na madhara ya sukari kwa mwili wa binadamu
Gazeti hilo limeripoti kuhusu Mwenyekiti wa chama cha wenye kisukari Tanzania, Prof Andrew Swai ambaye ametamani sukari iendelee kuadimika na bei yake kuwa juu ili matumizi yake yapungue kwa jamii kutokana na madhara ya bidhaa hiyo kwa mwili wa binadamu.
Gazeti hilo limesema Prof Swai ameyazungumza hayo jana jijini Dar es salaam wakati wa semina kwa waandishi wa habari iliyolenga kuelimisha juu ya magonjwa yasiyoambukiza Prof Swai ambaye ni daktari katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alisema matumizi ya sukari ni moja ya kichocheo cha magonhjwa yasiyoambukiza kama kisukari na shinikizo la damu
Prof Swai amenukuliwa na Gazeti la Habari Leo akisema…………….>>>‘Kwa upande wa sekta ya afya tunaona ni vizuri sukari kuadimika ndio maana nchi kama uingereza inapandisha bei ya sukari kuanzia mwakani ili kudhibiti matumizi makubwa ya sukari hivyo kuongeeka bei ni njia mojawapo ya kuzuia watu wasitumie’
Hata hivyo alisema anatambua kuadimika kwa sukari nchini hakutokani na sababu za kiafya lakini ni vyema serikali kuiga hatua kama ya Uingereza na nchi zilizoendelea za kupandisha bei vitu vinavyochangia magonjwa yasiyo ambukiza kama sukari, tumbaku na vileo
millard Ayo.
.
.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT