OBAMA KUTOHUDHURIA MAZISHI YA MUHAMMAD ALI. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Wednesday, 8 June 2016

OBAMA KUTOHUDHURIA MAZISHI YA MUHAMMAD ALI.

Image copyrightAP
Image captionObama kutohudhuria mazishi ya Muhammad Ali
Rais wa Marekani Barrack Obama hatohudhuria mazishi ya marehemu Muhammad Ali siku ya Ijumaa,kulingana na Ikulu ya rais.
Ali alifariki Ijumaa iliopita akiwa na umri wa miaka 74 katika hospitali moja huko Phoenix, Arizona.
Viongozi duniani watakuwa miongoni mwa maelfu watakaohudhuria mazishi hayo yatakayofanyika katika eneo la Louisville,Kentucky ambapo Ali alizaliwa.
Image copyright
Image captionObama
Ikulu ya White House imesema bw Obama na mkewe Ali, Lonnie walizungumza kwa njia ya simu.
Miongoni mwa wale watakaohudhuria ni rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na mfalme Abdullah wa Jordan.
Aliyekuwa bingwa wa ndondi katika uzani mzito duniani Lennox Lewis na muigizaji Will Smith ambaye aliigiza kama Ali ni miongoni mwa wale watakaobeba jeneza lake.
BBC
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT