MALAWI:MAUAJI YA ALBINO YAHOFIWA. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Tuesday, 7 June 2016

MALAWI:MAUAJI YA ALBINO YAHOFIWA.


Image copyrightGETTY
Image captionAlbino

Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Amnesty International, limeonya kutokea kwa wimbi jipya la mauwaji dhidi ya Albino nchini Malawi.
Umoja wa mataifa unakadiria kuwa visa 65 vya kutekwa kwa albino, kukatwakatwa viungo vyao au kuuwawa, vimeripotiwa nchini humo tangu mwaka 2014.
Amnesty, inasema kuwa watoto wa ulemavu wa ngozi, ndio walio kwenye hatari kubwa ya kuvamiwa au kutekwa nyara.

Image captionWatot albino ndio hulengwa zaidi

Watu hao wanawalenga, kwa sababu wachawi na madakatri wa kienyeji wanaamini kuwa sehemu ya viungo vya albino huleta baraka na utajiri iwapo vitatumika katika matambiko ya kitamaduni.
Amnesty inasema kuwa mashambulio dhidi yao yanaendelea licha ya serikali kupitisha sheria ya kuwapiga risasi wauwaji pindi wakipatikana kutekeleza uhalifu huo.
BBC
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT