June 17 2016 nimekutana na hii stori kuhusu kuanza kutengenezwa kwa Treni za kifahari na siku zitakazoanza kutumika chombo cha habari cha ‘CNN’ wametoa taarifa na headlines zikionyesha kuanza kutengenezwa kwa Treni za kifahari nchini Japan na kuanza kutumika May 2017 na hizi ndio zitakuwa Treni za kifahari zaidi duniani.
Treni hii ya Twilight Express Mizukaze ya JR Magharibi na treni ya Suite Shiki-Shimaya JR Mashariki zitakazo anza kufanya kazi rasmi May 2017, Treni hizi yenye uwezo wa kubeba abiria 30 na kua na wasimamizi 1o.
Treni hizo zitakuwa na madirisha ya vioo zitakavyoweza kuwaonyesha abiria nje na kupata nafasi ya kuona maeneo yote kama Osaka na Shimonoseki,Miyajima, bahari ya Japan, Mlima Daisen na Seto na visiwa vya bahari ya Inland ambavyo vitaweza kuwapa fursa ya kuweza kupiga picha.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT