TCRA YATOA MAFUNZO YA MATUMIZI YA HUDUMA ZA MITANDAO KWA WIZARA YA HABARI. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Friday, 6 May 2016

TCRA YATOA MAFUNZO YA MATUMIZI YA HUDUMA ZA MITANDAO KWA WIZARA YA HABARI.

TC1
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaana Michezo Bi.Nuru Khalfani Mrisho akizungumza  wakati akifungua  mafunzo mafupi ya matumizi ya huduma za mawasiliano na mitandao ya kijamii yanayotolewa kwa watumishi wa wizara ya habari,utamaduni,Sanaa na michezo.Wengine
TC2
Meneja Mawasiliano Mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA) Bw.Innocent Mungy akitoa mada ya ukuaji wa sekta ya mawasiliano na changamoto zake kwa watumishi wa umma kutoka wizara ya habari,utamaduni,Sanaa na Michezo leo jijini Dar es Salaam.
TC3
Kaimu Mkurugenzi Mamlakaya Mawasiliano Tanzania(TCRA)Mhandishi James Kilaba  akizungumzana katika warsha hiyo iliyofunguliwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaana Michezo Bi.Nuru Khalfani Mrisho.
TC4
Watumishi wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaana Michezo wakifuatilia kwa karibu mafunzo ya Matumizi Mazuri ya huduma za  Mawasiliano na mitandao ya kijamii iliyotolewa leo hii na mamlaka ya Utangazaji Tanzania.(P.T)
Na Jacquiline Mrisho MAELEZO
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa mafunzo ya matumizi ya huduma za mawasiliano kwa watumishi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kupata muongozo utakaowasaidia kuepuka matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.
Akifungua mafunzo hayo ya siku moja yaliyofanyika leo Jijini Dar es salaam, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Nuru Mllao amewataka watumishi wa wizara hiyo kuzingatia mafunzo hayo ili kuepuka matatizo ya mitandao ya kijamii wakati wakuteleza majukumu yao.
“Tumegundua kwamba watumishi wanahitaji muongozo juu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii, hivyo tunashukuru sana uongozi wa TCRA kukubali kutoa mafunzo kwa watumishi wetu”alisema Bi.Nuru.
Aidha Bi Nuru ametoa rai kwa TCRA kutoa mafunzo hayo kwa watumishi wa wizara nyingine kwa kuwa watumishi wote wanatakiwa kupata miongozo juu ya matumizi sahihi na usalama wa huduma hizo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi James Kilaba, alisema kuwa matumizi ya mitandao ya kijamii yameongezeka hivyo kuchangia kuongezeka kwa changamoto za matumizi mabaya ya mitandao hiyo.
Kwa upande wa huduma za mawasiliano ya simu, Mhandisi Kilaba alisema kuwa mawasiliano ya simu yanakua kwa kasi nchini hali ambayo inaongeza matumizi mabaya ya mawasiliano ya simu.
“Idadi ya laini za simu kwa miaka 12 iliyopita ilikuwa ni milioni 2.3 lakini hadi kufikia mwezi Machi mwaka huu idadi ya laini ni takribani milioni 40, wananchi ni wengi wanaotumia huduma za mitandao na wengi wao wanaitumia vibaya”alisema Muhandisi Kilaba.
Mhandisi Kilaba alielezea kuwa mafunzo hayo yataegemea kwenye nyanja za kukua kwa sekta ya mawasiliano na changamoto zake pamoja na mambo muhimu ya kuzingatia katika matumizi ya mitandao ya kijamii.
Alisisitiza kuwa kupitia mafunzo hayo watumishi wataweza kujua matumizi sahihi ya mitandao hasa katika shughuli zao za kiofisi.
Katika kuzingatia usalama wa mawasiliano yao, TCRA imewashauri watumishi pamoja na wananchi kwa ujumla kutotumia nywila (password) moja kujiunga kwenye mtandao zaidi ya mmoja.
Aliwataka kutoweka nywila ambazo zinahusisha mambo binafsi ambayo yanajulikana kwa watu wengi ili kuzuia mtu mwingine asipate urahisi wa kubuni kuingia katika mtandao wa mtu mwingine.
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT