Mei 6 2016 bunge linaendelea tena Dodoma, katika kipindi cha maswali na majibu Mbunge wa Bukombe Doto Biteko ameuliza Serikali kuwa ‘Je, kwanini Serikali inachukua muda mrefu sana kurekebisha mishahara ya Walimu baada ya kupandishwa vyeo?‘
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejiment ya utumishi wa Umma na Utawala bora >>>’Ni
kweli kwamba miaka ya nyuma kulikuwepo ucheleweshwaji wa kurekebisha
mishahara kwa mfumo wa taarifa za kiutumishi na mishahara wakati huo
kila mwajiri kuwasilisha marekebisho ya watumishi wake Ofisi ya Rais‘
‘Kuanzia
mwaka 2012 mfumo huu wa taarifa za kiutumishi na mishahara uliimarishwa
kutoka toleo la 7 kwenda la 9 la Lawson ambapo mwajiri alisogezewa
huduma ya kufanya marekebisho mbalimbali ya kiutumishi yanayotokea
katika ofisi yake bila ya kulazimika kusafiri kwenda Dar es salaam‘
‘Pamoja
na utaratibu huu mzuri, mazingira machache yanayoweza kuchelewesha
marekebisho ya mishahara kufanyika kwa wakati kutokana na kuingizwa
taarifa za watumishi kwenye mfumo baada ya orodha ya malipo ya mishahara
katika mwezi husika kufungwa‘
‘Napenda kupitia Bunge hili, kuwataka waajiri wote kufanya marekebisho ili kuepusha ucheleweshaji wa haki za Watumishi.’
MILLARD AYO.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT