Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha
Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza katika
Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza
Dkt. Asha-Rose Migiro mara baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania
nchini Uingereza katika Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika
picha na Dkt. Asha-Rose Migiro Balozi wa Tanzania nchini Uingereza,
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
John Kijazi katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia
jambo na Dkt. Asha-Rose Migiro Balozi wa Tanzania nchini Uingereza
pamoja na Profesa Cjanaphas Migiro mme wa Dkt. Asha-Rose mara baada ya
tukio la uapisho katika Ikulu ndogo ya Chwamwino mkoani Dodoma.(P.T)
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
jambo na Dkt. Asha-Rose Migiro Balozi wa Tanzania nchini Uingereza huku
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje
Balozi Augustine Mahiga wakisikiliza.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia
jambo na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya kutoka kwenye
tukio la kumuapisha Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa Balozi mpya nchini
Uingereza . PICHA NA IKULU
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha
Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.
Hafla ya
kuapishwa kwa Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro imefanyika jana tarehe 05
Mei, 2016 katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma, na kuhudhuriwa
na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan.
Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Peter Kallaghe ambaye amerudishwa nyumbani.
Akizungumza
baada ya kuapishwa, Dkt. Migiro ameahidi utumishi uliotukuka na kwamba
atahakikisha uhusiano na ushirikiano mzuri na wa kihistoria uliopo kati
ya Tanzania na Uingereza unaimarishwa zaidi, hususani katika kuvutia
uwekezaji, biashara na utalii baina ya nchi hizi mbili.
Dkt.
Migiro pia ametoa wito kwa watanzania waliopo hapa nchini na waishio
Uingereza kuitumia ofisi hiyo ya ubalozi ipasavyo, ili waweze kunufaika
na fursa mbalimbali hasa za kiuchumi.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
05 Mei, 2016
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT