Chama cha National league for Democracy nchini Myanmar kimewateua wagombea wawili huku taifa hilo likianza harakati za kumchagua rais mpya.
Wanahabari wanasema mmoja wao ni Htin Kyaw ambaye ana matumaini ya kuchaguliwa rais na chama cha NLD kinachodhibiti bunge.
Uteuzi huo unathibitisha kwamba kiongozi wa NLD Aung San Suu Kyi hatakuwa rais wa taifa hilo.Hata hivyo bi Suu Kyi amekuwa akisema kuwa atakuwa juu ya rais.
Licha ya ushindi wake mkubwa katika uchaguzi,Aung San Suu Kyi alishindwa kulishawishi jeshi kwamba anaweza kuwa rais.
Kipengele 59 cha katiba kinamzuia kuwa rais kwa sababu wanawe wana pasipoti za Uingereza na sio za Burma,hivyobasi amelazimika kuchagua mtu mwengine kuchukua mahala pake.
Na mtu huyo ni Htin Kyaw aliyekuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Oxford ambaye amemjua maisha yake yote.
Ni mwanachama shupavu wa NLD na amekuwa mwandani wake wa karibu tangu Suu Kyi alipowachiliwa kutoka kifungoi chake cha nyumbani.
bbc swahili.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT